Teknolojia Mpya Polisi wa China Wanayo Tumia Kukamata Wahalifu

Sasa wahalifu kukamatwa nchini china kwa kutumia miwani
Teknolojia mpya ya miwani china Teknolojia mpya ya miwani china

Nchini China, teknolojia kwa upande wa polisi imezidi kuwa kubwa sana na kurahisishia kazi kwa polisi wa nchini humo hasa pale linapokuja swala la kukamata wahalifu haswa wanao ingia na kutoka nchini humo.

Teknolojia hiyo mpya inayo husisha miwani maalum zenye teknolojia ya kutambua uso (facial recognition) zinauwezo wa kutambua baadhi ya wahalifu kupitia kifaa maalum ambacho huangalia sura ya mtuhumiwa na kuwasilisha kwenye datakazi (database) ya wahalifu na mara moja polisi hupewa taarifa kuhusu mtuhumiwa na hatimaye mtuhumiwa huyo kukamatwa.

Kwa mujibu wa tovuti ya People’s Daily ya nchini humo, tayari teknolojia hiyo imewezesha kukamata wahalifu mbalimbali wanao husishwa na makosa makubwa ya uhalifu nchini humo zaidi ya 26 pamoja na wahalifu wengine wanao ingia kwenye nchi hiyo kwa majina pamoja na hati za kusafiria za kugushi.

Advertisement

Kampuni inayohusika na utengenezaji wa miwani hizo, LLVision Technology Co. kupitia msemaji wake imesema kuwa teknolojia hiyo mpya ina uwezo wa kuangalia utambulisho wa watu kutoka kwenye datakazi (database) ya watu zaidi ya 10,000 na kurudisha majibu kwa haraka ndani ya sekunde 0.1 hivyo kufanya miwani hizo kuwa na uharaka zaidi pale inapo hitajika ku-mtambua muhalifu kwa haraka bila kumuangalia sana kwa muda mrefu.

Kampuni hiyo ambayo imebobea kwenye utengeneza wa vifaa vya kutambua uso (facial recognition) imesema teknolojia hiyo kwa sasa bado iko kwenye majaribio na haitapatika kwa wateja wengine kutokana na hofu ya usalama wa usiri inayotokana na teknolojia hiyo.

Kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya Teknolojia, Pakua sasa App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia unaweza kujiunga na Channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili kujifunza mambo yote ya Teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use