Baada ya mkutano wa #MWC 2018 au Mobile World Congress 2018 kufunguliwa rasmi hapo siku ya jana bado kampuni mbalimbali zimendelea kuonyesha teknolojia zake mpya zitako ufungua mwaka 2018. Kampuni ya Nokia nayo haikuwa nyuma kwani mwaka huu kampuni hiyo imekuja na simu zake mpya 5.
Ikiwa inasaidia kutengeneza simu zake na kampuni kutoka Finland ya HMD Global, Nokia sasa imekuja na simu mpya za Nokia 9, Nokia 8 Pro, Nokia 7 Plus pamoja na Nokia 4. Sasa ili uweze kuzifahamu simu hizi kwa undani zaidi twende tuka angalie simu moja baada ya nyingine.
Nokia 8110 4G
Mwaka jana kwenye mkutano wa MWC 2017 kampuni ya Nokia ilikuja na simu ya Nokia 3310 ambayo ilikuwa ni toleo jipya la simu ya zamani kutoka kampuni hiyo, mwaka huu Nokia pia imerudi na toleo jipya la simu ya zamani iliyo jizolea umaarufu hasa kwenye filamu ya “The Matrix” ya mwaka 1999 kwa kutumiwa sana na muigizaji maarufu kwenye filamu hiyo. Kuwa maarufu huku kumefanya simu hii kuitwa jina la The Matrix na baadhi ya watumiaji au wapenzi wa simu hiyo kwenye miaka ya 1999.
Sasa leo kampuni ya Nokia imerudisha simu hii yenye vibonyezo vinavyo fichika kwa kusogeza mfuniko maalum kwenye vibonyezo hivyo. Hakika ni mtindo wa siku nyingi sana lakini Nokia wamerudisha mtindo huu sokoni kwa kuja na simu hii ya Nokia 8110 yenye uwezo wa 4G pamoja na sifa zingine kama zifuatavyo.
Sifa za Nokia 8110 4G
- Mfumo wa uendeshaji – Nokia Smart Feature OS
- Uwezo wa Processor – Dual-core 1.1GHz Qualcomm 205 processor
- Uwezo wa Kamera – Ina kamera ya Megapixel 2
- Uwezo wa RAM – 512MB RAM
- Ukubwa wa Ndani – 4GB internal storage
- Ukubwa wa Kioo – 2.4-inch, 320×240-pixel display
- Uwezo wa Battery – 1,500 mAh battery
- Mengineyo – Inatumia sehemu ya Micro-USB kwaajili ya kuchaji, inatumia line aina ya Micro SIM, Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama 3.5mm headphone jack, Inayo FM Radio.
- Bei – Simu hii imepangwa kuuzwa kwa dollar za marekani $100 ambayo ni sawa na Tsh 225,000 (kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya leo) kumbuka kwa Tanzania bei inaweza kubadilika.
- Upatikanaji – Simu hii inategemewa Kuanza kupatikana Kuanzia mwezi May (mwezi wa tano) mwaka huu 2018.
Nokia 8 Sirocco
Nokia 8 Sirocco ni simu mpya kutoka kampuni ya Nokia, simu hii ni moja kati ya simu inayo vutia zaidi kutoka kampuni ya Nokia. Wakati kampuni nyingine za simu zikitumia Aluminium kutengeneza simu zake, kampuni ya Nokia imepita njia yake yenyewe kwa kuja na simu hii iliyotengenezwa kwa Stainless Steel. Kwa upande wa sifa simu hii haijatofautia sana na Simu ya Nokia 8 ya mwaka jana lakini badala yake simu hii imeboreshwa zaidi kwenye muonekano.
Sifa za Nokia 8 Sirrocco
- Ukubwa wa Kioo – inch 5.5 chenye teknolojia ya 2K display
- Uwezo wa Processor – Qualcomm Snapdragon 835 processor
- Uwezo wa RAM – 8GB RAM,
- Ukubwa wa Ndani – 128GB storage yenye uwezo wa kuongezwa kwa kutumia microSD card
- Uwezo wa Kamera – Ina kamera mbili nyuma moja ina Megapixel 12 na nyingine ina Megapixel 13, Kamera ya mbele ni megapixel 5
- Mfumo wa Uendeshaji – Android Oreo One
- Uwezo wa Battery – 3,260 mAh battery
- Mengineyo – Inauwezo wa kuzuia maji IP67 rated waterproof
- Bei – Simu hii inategemewa kuuzwa kwa dollar za marekani $925 sawa na Tsh 2,090,000
- Upatikanaji – Simu hii itanza kupatikana nchini Australia kwanza kuanzia mwezi wa Nne (kwenye inchi zingine mpaka itakapo tangazwa)
Nokia 7 Plus
Nokia 7 Plus ni simu nyingine mpya kutoka Nokia simu hii pia imekuja na maboresho kadhaa kutoka kwenye simu ya Nokia 7 ya mwaka jana simu hii inakuja na –
Sifa za Nokia 7 Plus
- Ukubwa Kioo – 6-inch display yenye resolution ya 2,160×1,080
- Uwezo wa Processor – Qualcomm Snapdragon 660 processor
- Ukubwa wa RAM – 4GB RAM, 64GB storage
- Uwezo wa Kamera – Ziko mbili moja ina Megapixel 12 na nyingine Megapixel 13 telephoto lens, Kamera ya mbele Megapixel 16
- Uwezo wa Batterty – 3,600mAh non-removable battery with fast charging
- Mfumo wa Uendeshaji – Android Oreo One
- Bei – Simu hii inategemewa kupatikana kwa dollar za marekani $490 sawa na Tsh 1,102,010 ( kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya leo)
- Upatikanaji – Inategemewa kuanza kupatikana kuanzia Mwezi April mwaka huu 2018.
Nokia 6 (2018)
Nokia 6 pia ni simu mpya kutoka kampuni ya nokia na kama ilivyo simu ya nokia 7 plus simu hii inakuja na maboresho mapya na inakuja ikiwa inauzwa kwa bei nafuu kidogo ukilinganisha na simu mpya ya nokia 7 plus.
Sifa za Nokia 6 (2018)
- Ukubwa wa Kioo – 5.5-inch display yenye resolution ya 1,920×1,080-pixel
- Uwezo wa Processor – Qualcomm Snapdragon 630 processor
- Uwezo wa RAM – Ziko za aina mbili GB 3 au GB 4
- Ukubwa wa Ndani – Ziko za aina mbili GB 32 au GB 64
- Uwezo wa Kamera – Kamera ya nyuma Megapixel 16 kamera ya mbele Megapixel 8
- Uwezo wa Battery – 3,000mAh non-removable batter
- Bei – Simu hii inatarajia kupatika kwa dollar za marekani $280 sawa na Tsh 629,720 (kwa mujibu wa viwango vya fedha vya leo) bei inaweza kubadilika kwa Tanzania.
- Mengineyo – Inatumia sehemu ya USB Type-C pia inayo mfumo wa fast charging
- Upatikanaji – Kuanzia mwezi wa Nnne mwaka huu 2018.
Nokia 1
Nokia 1 ni moja kati ya simu zilizo tolewa na nokia mwaka huu 2018, simu hii imetengenezwa maalumu kwa wale watu wanao itaji kupiga simu na kupokea pekee pamoja na kufanya mambo ya kawaida. Simu hii pia ni moja kati ya simu za bei nafuu sana na zinakuja na mfumo wa Android Go ambao umeboreshwa kwaajili ya simu ambazo hazina uwezo mkubwa.
Sifa za Nokia 1
- Ukubwa wa Kioo – 4.5-inch display
- Uwezo wa Processor – Quadcore 1.1GHz processor
- Ukubwa wa Ndani – 8GB storage (inayoweza kuongezeka kwa memory card hadi ya 128GB)
- Uwezo wa Kamera – Kamera ya nyuma megapixel 5 yenye LED flash, Kamera ya mbele megapixel 2
- Mfumo wa Uendeshaji – Android Oreo Go
- Uwezo wa Battery – 2,150 mAh battery yenye uwezo wa kutoka
- Mengineyo – Programu zote za Android Go zinafanya, sehemu mbili za kuweka line, pia inayo Music player na FM radio
- Bei – Simu hii inategemewa kuuzwa kwa dollar za marekani $85 sawa na Tsh191,165
- Upatikanaji – Inategemwa kupatikana kuanzia mwishoni mwa mwezi wa nne mwaka huu 2018
Na hizo ndio simu mpya kutoka kampuni ya Nokia mwaka huu 2018, endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujuza yale yote yatakayo endelea kujiri kwenye mkutano wa MWC 2018 au Mobie World Congress unao endelea kufanyika huko nchini Barcelona. Pia unaweza kutembelea ukurasa wetu wa #MWC 2018 kujua yote yalio jiri na yatakayo jiri.
Naomba bei jumla simu zote za nokia za batani na smartphone
naomba bei ya simu ya batani