Kampuni ya Samsung Yazindua Hard Disk Kubwa ya Terabyte 30

Samsung yavunja rekodi kwa kuja na hard disk kubwa zaidi mpaka sasa
Kampuni ya Samsung Yazindua Hard Disk Kubwa ya Terabyte 30 Kampuni ya Samsung Yazindua Hard Disk Kubwa ya Terabyte 30

Kampuni ya Samsung yenye makao yake makuu nchini Korea ya Kusini hivi leo imevunja rekodi nyingine tana kwa kuja na Hard Disk kubwa kuliko zote duniani, Hard disk hii ya aina ya SSD au Solid-state drive ina uwezo au ukubwa wa Terabyte (TB) 30 ambayo ni sawa na GB 30,000.

Hard Disk hiyo imetengenezwa kwa vitufe maalum vinavyoitwa NAND ambavyo vipo zaidi ya 30 ambapo kila kitufe kimoja kina uwezo wa terabyte 1 TB ambavyo ni sawa na kusema hard disk hiyo inauwezo wa kuhifadhi filamu za HD za ukubwa wa GB 1 zaidi ya filamu 5,700 au zaidi.

Mwaka 2016 Samsung ilizindua hard disk nyingine ambayo ilikuwa kubwa zaidi kwa kipindi hicho ambapo hard disk hiyo ilikuwa na uwezo wa TB 16 sawa na GB 16,000, lakini pia kampuni ya Seagate ilisha kuja na Hard Disk ya TB 60 ambayo haiku fanikiwa kuwafikia wanunuzi na ilikuwa kama sehemu ya maonyesho pekee ukitofautisha na Hard Disk hii ya Samsung.

Advertisement

Mbali na uwezo wake mkubwa wa TB 30 hard disk hii inakupa uwezo wa kuhifadhi vitu na kunakili vitu kwa speed ya MB 2,100 kwa sekunde ambayo ni sawa na kusema ndani ya sekunde moja unaweza kutuma filamu yenye ukubwa wa GB 2. Uwezo huu ni mara tatu zaidi ya uwezo wa hard disk za kawaida za SSD ambazo utazikuta kwenye laptop mbalimbali.

Update Tarehe 20/3/2018 :  Hard Disk kubwa kuliko zote sasa ni ya Terabtye 100 kutoka Nimbus.

Hard disk hiyo iliyopewa jina la PM1643, inasemekana kuja na warrant ya miaka mitano yani maana yake ni kuwa ikiharibika ndani ya miaka mitano unaweza kupewa nyingine au kufanyiwa marekebisho. Hii inaonyesha kuwa samsung inajiamini sana kwenye utengenezaji wa Hard Disk hiyo. Kuhusu bei bado haijajulikana lakini ukweli ni kuwa haitakua bei rahisi… endelea kutembelea Tanzania Tech kujua zaidi…

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use