Hivi karibuni kampuni ya Google kupitia soko la progarmu za simu la Play Store ita-anza kupokea malipo ya kununua baadhi ya programu mbalimbali ndani ya soko hilo kwa kutumia mfumo wa malipo wa Mpesa huko nchini Kenya.
Kupitia muungano wa kampuni ya Simu ya Safaricom ambayo ndio watoaji wa huduma za Mpesa nchini Kenya na kampuni ya DOCOMO Digital ya nchini London, sasa watengenezaji wa programu wataweza kuuza programu zao kwa urahisi zaidi hata kwa wale watu ambao hawana kadi ya manunuzi kwa bank maarufu kama credit cards.
Bado haijajulikana lini sehemu hii itanza kufanya kazi rasmi nchini kenya, lakini labda tutegemee sehemu hiyo kuanza kutumika kabla ya mwisho wa mwezi wa nne au watano mwaka huu 2018. Kuhusu huduma hii kufika Tanzania bado hakuna taarifa zozote juu ya hili pengine tuendelee kusubiri labda Vodacom Tanzania itafikiria kuleta huduma hizi hapa Tanzania siku za karibuni.
Update tarehe 9 March 2018 – Google imeruhusu Tanzania Kuanza Kuuza App kupitia Soko la Play Store, kipindi cha nyuma ilikubidi kuweka app za bure pekee kwenye soko hilo lakini sasa unaweza kuweka app za kununua.