Picha Nyingine ya Samsung Galaxy S9 Imevuja (Muonekano Mpya)

Huu ndio muonekano wa Samsung Galaxy S9 kwa nyuma
samsung-galaxy-s9 samsung-galaxy-s9

Ni siku nyingine tena habari za simu mpya ya Samsung Galaxy S9 zimezidi kuwa nyingi wakati tukielekea kwenye uzinduzi wa simu hiyo mpya tarehe 25 mwezi huu.

Katika kuhakikisha hupitwi na habari zinazo husu simu hiyo, leo nimekuletea muonekano mpya wa simu hiyo mpya kabla ya kutoka kwake au kuzinduliwa kwake, picha hii inaonyesha uso wa nyuma wa simu hii ambao tulikua bado hatujawahi kuona.

Advertisement

Samsung inategemea kufanya maboresho makubwa kwenye kamera za simu yake ikiwa pamoja na kuongeza uwezo wa kamera hizo kupiga picha vizuri kwenye mwanga mdogo pamoja na hata wakati wa usiku.

Zimebaki siku chache mpaka kujua kwa uhakika ni kitu gani Samsung wameongeza kwenye simu hizi lakini kwa ufupi simu hii inategemewa kuja na sifa kama hizi zifuatazao

  • Kioo cha – Inch 5.8in / 6.2in QHD+ Super AMOLED curved display (570ppi / 529ppi)
  • Processor ya –  Qualcomm Snapdragon 845 (US) / Samsung Exynos 9810 (UK)
  • Uwezo wa RAM –  4GB RAM or 6GB RAM / 6GB RAM
  • Ukubwa wa Ndani –  64GB/128GB / 64GB/128GB/256GB storage
  • Uwezo wa Kamera –  Kamera ya Nyuma 12MP Dual Pixel camera with OIS (f/1.5, f/2.4) / Vertical dual rear-facing camera, Kamera ya Mbele Mega pixel 8.

Kwa ufupi tu, hizo ndio baadhi ya sifa ambazo zinategemewa kuja kwenye simu ya Samsung Galaxy S9. Kujua zaidi endelea kutembelea Tanzania Tech tutaendelea ku-katarifu pale tutakapo pata habari zaidi za simu hii.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use