Bitcoin ni moja kati ya jina maarufu sana siku hizi karibia kila mtu anae fuatilia mambo ya mtandao lazima atakuwa anajua kuhusu Bitcoin. Sasa kukupa ujuzi zaidi kuhusu hili leo nime kuandalia mambo kadhaa ambayo inawezekana hujui kuhusu Bitcoin.
1. Bitcoin ni nini.?
Kwanza turudi nyuma kidogo na tuanze na Bitcoin ni nini.? kwa wale msiojua bitcoin huu ni mfumo wa malipo ya pesa za kimtandao ambao hausishi bank, yaani hapa namaanisha Bitcoin ni aina ya pesa za kidigital ambazo haziitaji bank ili kuongeza au kupunguza dhamani.
2. Muanzilishi wa Bitcoin Hajulikani Mpaka Leo
Bitcoin ilianzishwa mwaka 2009 na mtu asiye julikana, lakini wataalamu wa mambo wanasema jina linalo jilikana mpaka sasa la muanzilishi huyo ni Satoshi Nakamoto, bado hakuna aliye na uhakika kwenye hili na mtu huyu mpaka leo hii ameamua kuto kujulikana na kwa mujibu wa makala kwenye mtandao wa Media, ni NSA (National Security Agency) au shirika la usalama la marekani pekee ndio wanajua utambulisho halisi wa mtu huyo. (hili pia halina uhakika)
3. Bitcoin Haiwezekani Kukamatwa na Sheria
Tofauti na mifumo mingine ya pesa ambayo inaweza kushikiliwa na serikali au kuzuiwa Bitcoin haiwezekani kushikiliwa na serikali kwani mfumo huu wa pesa ni wakidigitali na huwa kwenye programu maalum inayo julikana kama (wallet) ambayo inamilikiwa na mtu mwenye. Kwa mujibu wa tovuti ya washingtonpost bitcoin inapendelewa kutumiwa zaidi na watu wanaotaka kuepuka sheria na hasa wale wanaofanya biashara haramu, lakini pia bado hakuna ushaidi kwenye hili.
4. China Serikali imekataza Kununua na Kuuza Bitcoin
China ni moja ya nchi ambazo zimepiga marufuku uuzaji na ununuaji wa Bitcoin, hata hivyo jitihada hizo bado hazija zaa matunda kwani bado wananchi wa nchini humo wanatumia bitcoin. Nchi nyingine ambazo bitcoin hairuhusiwi ni Saudi Arabia, Bolivia, Kazakhstan, Ecuador pamoja na Bangladesh.
5. Bitcoin inamaliza Umeme
Bitcoin inaweza kuzalishwa kwa kutumia kompyuta na kwa mujibu wa tovuti ya arstechnica bitcoin inatumia umeme kiasi kikubwa yani zaidi ya nchi ya Denmark ambayo ndio inasemekana inatumia umeme zaidi kuliko nchi zote duniani. Kwa mujibu wa tovuti hiyo kiasi cha umeme kinacho tumika kukamilisha biashara ya Bicoin kwa mwaka ni sawa na 32TWh.
6. Tajiri Mkubwa Kuliko Wote Duniani wa Bitcoin
Tajiri mkubwa kuliko wote duniani wa mfumo huu wa bitcoin anasemekana kuwa ni Satoshi Nakamoto, ambaye ndie muanzilishi wa Mfumo huu, inasemekana muanzilishi huyo anamiliki bitcoin zaidi ya milioni moja ambazo zina thamani ya dollar za marekani $8,396,045,000 bilioni.
Na hayo ndio baadhi ya mambo ambayo nimekuandalia leo kuhusu Bitcoin, ili kujua zaidi kuhusu Bitcoin endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujuza zaidi kuhusu hili pamoja na jinsi ya kununua Bitcoin na uhalali wake hapa Tanzania.
Mwanzilishi wa bitcoin ni Mzee Sanitoshi Nakamoto mjapani jeuri wa technology, alianza kuibunibuni mwaka 2006 ilipofika mwaka 2009 akaanza kuitangaza mitandaoni.
Kauli ya :-
“MGUNDUZI WA BITCOIN HAJULIKANI MPAKA SASA” Ifutilie mbali kabla wajanja hawajakucheka.
Hilo sio jina halisi la aliyegundua Bitcoin. go do your home work tunafanya utafiti kabla ya kuandika makala.
Satoshi Nakamoto is the name used by the unknown person or people who designed bitcoin and created its original reference implementation. As part of the implementation, they also devised the first blockchain database.
wale wanao predict bei za Bitcoin wanatumia technology ipi
Maoni*NAKUANZA BITCOIN, ILA NINA WASI WASI NITAAMINI VIPI KAM SIO WIZI WA MTANDAONI?
Naomba unisaidie jinsi ya kutumia bit con Kama na taka kuitumia kutolea pesa mtandaoni nimeambiwa nitumie paypal au bit con na PayPal kwa Tanzania hatulusiwi kupokea pesa nifanyeje