in

Jaribu App Mpya ya Google Relpy Kwenye Simu Yako ya Android

Sasa unaweza kujaribu programu ya Reply, download hapo chini

Google Reply

Hivi karibuni kampuni ya Google ilitangaza kuja na programu yake mpya ya Google Reply programu hiyo ambayo ni maalum kwaajili ya watumiaji wa simu za Android. Inakuja ikiwa inatumia mfumo wa AI au Artificial Intelligence kuweza kukusaidia kubuni majibu ya meseji zako bila wewe kuandika.

Jinsi programu hiyo inavyo fanya kazi ni kuwa, baada ya kupakua na kuinstall app hiyo itaongeza sehemu maalum ya Google Reply kwenye programu zako za kuchati za Google Allo, Whatsapp, Facebook Messenger, Android Messages, Skype, Twitter DMs, pamoja na Slack, sehemu hiyo itakuwa inakuletea mapendekezo ya majibu ya meseji mbalimbali utakazo tumiwa kabla wewe kuandika majibu ya meseji uliyotumiwa.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Baada ya kuchunguza proramu ya majaribio nimegundua kuwa programu hiyo inafanya kazi vizuri iwapo unatumia lugha ya kingereza na sio lugha nyingine, mbali na hapo programu hiyo inafanya kazi vizuri sana na inarahisisha pale unapokuwa unachat na mtu kwa lugha ya kingereza.

Unaweza kujaribu programu hii kwenye simu yako ya Android kwa kupakua programu hiyo kupitia HAPA, kumbuka kwa sasa programu hii inafanyiwa majaribio kwa watu wa chache na bado haipatikani kwenye soko la Play Store hivyo ni muhimu kupakua programu hiyo hapo juu kwa sasa.

Jaribu App Mpya ya Google Relpy Kwenye Simu Yako ya Android
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Hizi Hapa Browser Bora Zenye Mfumo wa Akili Bandia (AI)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.