in

Google Kuja na Kisakuzi cha Chrome Kinachozuia Matangazo

Sasa sema kwaheri kwa matangazo ya Pop ups Ads na mengine

Google Kuja na Kisakuzi cha Chrome Kinachozuia Matangazo

Hivi karibuni Google ilitangaza kuwa inafanyia kazi kisakuzi kipya cha Chrome ambacho kitakuwa na uwezo wa kuzuia aina fulani ya matangazo. Sasa hivi leo Google imetangaza kuwa kisakuzi hicho kipo tayari na kitaanza kutumika rasmi kuanzia siku ya kesho.

Matangazo ambayo yatazuiwa na kisakuzi hicho kipya cha Chrome ni kama yale matangazo ya pop up, matangazo yanayo toa sauti, matangazo yaliyozidi kwenye tovuti pamoja na matangazo mengine mengi ambayo hayaja kidhi vigezo na mashari ya Coalition for Better Ads.

Hii ni habari mbaya kwa watu wenye tovuti ambazo zina matangazo ya aina hii, ukizingatia Google pia imeanzisha sehemu mpya ambayo itakuwa kwenye tovuti ya Google Search Console ambayo ni maalum kwa watu wenye tovuti, sehemu hii italazimisha tovuti kuangaliwa na Google kama tovuti ina kidhi vigezo na mashari ya utangazaji hii ikiwa pamoja na kuangalia vigezo na masharti ya Coalition for Better Ads.

Kiasakuzi cha Google Chrome ni moja kati ya visakuzi vinavyotumiwa na watu wengi zaidi, hivyo lazima sehemu hii mpya italeta mabadiliko makubwa kwenye matangazo ndani ya tovuti mbalimbali. Kwa taarifa zaidi kuhusu sehemu hiyo ya kuzuia matangazo itakavyo fanya kazi unaweza kusoma HAPA.

Twitter Kuanza Tena Kuthibitisha Akaunti (Verified Badge) 2021
Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.