in

Jaribu App ya Tanzania Tech ya Android Kabla Haija Toka Rasmi

Jaribu sehemu mpya za programu ya Tanzania Tech kabla ya kutoka

App ya Android ya Tanzania Tech

Habari za muda huu wapenzi wa teknolojia, leo ningependa kuwa karibisha kujaribu App yetu mpya ya Tanzania Tech kwa mfumo wa Android. App hii mpya ina maboresho mengi sana lakini moja kati ya maboresho makubwa ni uwezo wa kusoma App hii wakati wa usiku bila ku-umiza macho yako.

App hii mpya ya sasa Mbali na kuwa na uwezo bora lakini imezingatia vigezo na mashari ya Google ikiwa pamoja na kuacha kufanya kazi kwenye vifaa vya zamani. Sasa hapa tumefanya mambo mawili makubwa. App ya sasa itanza kufanya kazi kwenye vifaa vya Android 5.0 na kuendelea.

Hii ni kwa sababu kwa mujibu wa Google, programu nyingi pamoja na uwezo wa kutengeneza App bora huanzia kwenye vifaa fulani hii ni kutokana na kuongezwa kwa vitu vipya ambavyo ushindwa kufanya kazi vizuri kwenye simu za zamani.

Unaweza kupakua App hii mpya kupitia sehemu ya majaribio kwa kubofya hapo chini kisha bofya join alafu update programu yako.

JARIBU APP YA TANZANIA TECH

Apps za Kusaidia Kutuma SMS Nyingi kwa Pamoja (Android)

Kama una maoni yoyote au ushauri nini tubadilishe kwenye app yetu hii mpya unaweza kutuandikia maoni hapo chini, pia unaweza kuteandikia barua pepe kupitia [email protected].

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.