Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

App : Jaribu Programu Hizi Kwenye Simu Yako ya Android

Ongeza uwezo wa simu yako ya Android kwa kujaribu App hizi za Android
App : Jaribu Programu Hizi Kwenye Simu Yako ya Android App : Jaribu Programu Hizi Kwenye Simu Yako ya Android

Kupitia Tanzania Tech tutakuwa tukiwaletea App mbalimbali ambazo tunahisi mnaweza kuzipenda na app hizi nyingi zitakuwa sio zile tulizo zoea kuziona kila siku bali tutajitahidi kuwaletea App ambazo ni maarufu na ambazo ni bora kuwa nazo kwenye simu yako. Kwa kuanza leo nimekuandalia App hizi 5 ambazo na uhakika utazipenda au zitaweza kukusaidia kwa namna moja au nyingine.

1. Selfie Flash – bright pictures with any camera app

App hii ni bora kama simu yako haina kamera ya mbele na kama unapenda kupiga picha za Selfie wakati wa usiku basi app hii itakufaa sana tofauti na App zingine, app hii ya Selfie Flash ni bora sana na inakupa mwanga na kufanya picha zako kuwa angavu hasa wakati wa usiku.

Advertisement

2. Flip Browser (Light & Fast)

Programu hii inafanya kazi tofauti na visakuzi vingine ambavyo umezoea, kwani Flip Browser inafanya kazi vizuri pale unapokuwa kwenye mitandao ya kijamii na umekutana na link ya makala fulani na unataka kusoma makala hiyo bila kutoka kwenye mtandao husika. Flip Browser itakupa uwezo huo na utaweza kufungua link yoyote bila kutoka kwenye akunti yako ya mitandao ya kijamii.

3. Finger Security

FingerSecurity
Price: Free

App hii ni kwaajili ya wale wenye simu zenye sehemu ya Fingerprint, App hii itakusaidia endapo unataka kuweka ulinzi kwenye Programu mbalimbali za simu yako kwa kutumia Fingerprint. Wote tunajua kuwa sehemu ya fingerprint kwenye simu haiji na uwezo wa kufunga programu kama WhatsApp, Facebook au hata SMS, lakini kwa kutumia App hii utaweza kuweka ulinzi wa Fingerprnt kwenye kila eneo la programu za simu yako.

4. Feedster – News aggregator with smart features

App hii itakusaidia kusogeza akaunti zako zote za mitandao ya kijamii kwenye App moja, yani hapa kama unataka kukaa karibu na mitandao yako yote ya kijamii ndani ya App moja basi jaribu app hii.

5. WhatsRemoved

WhatsRemoved
Price: Free

Hivi karibuni WhatsApp imeleta njia ambayo mtu anaweza kufuta meseji aliyokutumia kabla wewe hujaisoma, sasa App hii itakusaidia kusoma meseji ambazo mtu amefuta kabla wewe hujasoma. Zaidi ya hapo App hii inakusaidia kupata baadhi ya meseji na picha zilizo futika kwenye simu yako.

BONUS

6. JustWink Greeting Cards

Sasa hii ni kwaajili ya siku ya wapendanao, App hii itakusaidia kuweza kutengeneza kadi za aina mbalimbali na kutuma kwa mtu moja kwa kwa kutumia link maalum, App hii tofauti na App nyingine inakupa uwezo wa kutengeneza kadi jinsi unavyotaka na zaidi ni kuwa app hii inauwezo wa kuweka sauti kwenye kadi yako kabla haujaituma ili mtu aweze kupata ujumbe wako vizuri zaidi pale unapo mtumia kadi hii.

Na hizo ndio App ambazo nime kuandalia siku ya leo, unaweza kuendelea kutembea Tanzania Tech kila siku tutakuwa tukiwaletea makala za programu mbalimbali za Android bila kusahau iOS, kama umependa app hizi tuandikie maoni hapo chini ukituambia kwanini pia usisahau kupakua App ya Tanzania Tech ili kupata habari mpya za teknolojia kila siku.

7 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use