Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Apps# 3 : Jaribu App Nzuri Kwenye Simu Yako ya Android

Jaribu programu hizi kwenye simu yako ya Android
App bora App bora

Ni kweli kuwa soko la Play Store limejaa programu nyingi sana na kama umekua ukitafuta programu mbalimbali za Android basi unasoma makala sahihi, hapa tutaenda kuangalia programu mbalimbali bora za android zinazoweza kukusaidia kwa namna moja au nyingine.

1. Musixmatch – Lyrics for your music

Sasa App hii ni bora sana kwa wale wapenzi wa muziki na pila wale wanaopenda kuimba au karaoke, App hii inakupa uwezo mkubwa sana wa kuweza kuona mashairi ya nyimbo mbalimbali. Nimejaribu hata baadhi ya nyimbo za kiswahili na imekuwa ikileta mashairi hayo tena bila kukosea sana. Kitu cha muhimu unatakiwa kuhakikisha majina ya nyimbo hizo yameandikwa vizuri.

Advertisement

2. Auto Scroller

Auto Scroller
Price: Free+

Auto Scroller ni programu ambayo huenda haijulikani sana kutokana na kuwa na download chache lakini app hii ni moja kati ya app bora sana. Programu hii itakusaidia kuweza kusogeza kioo cha simu yako pale unapokuwa unapitia makala au mitandao mbalimbali. Yaani badala ya kupapasa kidole kwenye kioo cha simu yako kila mara app hii itakupa uwezo wa kusogeza maandishi juu au chini kwa urahisi. App hii itakusaidia sana kama labda ukiwa unasoma kitabu na utaki kupapasa kidole kwenye kioo cha simu yako kila saa au hata pale unaposoma makala kwenye tovuti mbalimbali.

3. Ditty

Ditty
Price: Free+

Ditty ni moja kati ya programu au app nzuri sana kutumia, kwa kutumia app hii unaweza kutengeneza maneno yoyote kuwa kwenye nyimbo na video. Yaani unachotakiwa kufanya ni kuandika maneno unayotaka kisha unachagua mdundo ambayo ipo ndani ya app hiyo na app hiyo itatengeneza nyimbo inayofutana na mdondo huko kwa kutumia maneno uliyo andika hapo awali, mbali na hayo App hii itatengeneza video yenye maneno hayo. App hii ni nzuri kwa wale wanofanya promotion mbalimbali hasa kwenye mitandao ya kijamii. Mfano wa App hiyo unaweza kuangalia video hii..

Download Tanzania Tech App Click the link on Bio

A post shared by TANZANIA TECH (@tanzaniatech_) on

4. X Home Bar – Free

X Home Bar
Price: Free

X Home Bar ni moja kati ya app bora kuwa nayo hasa kama moja ya vitufe kwenye simu yako vimeharibika, App hii itakusaidia kuweza kuongeza mstari maalum chini ya kioo chako ambao mtari huo utakuwa kukifanya kazi kama vitufe vya Back, Home pamoja na Multitask. Jaribu App hii sasa.

5. Grammarly Keyboard — Type with confidence

App hii ni msaada mkubwa hasa kwa wale wanaotaka kuandika meseji au ujumbe wowote kwa kingereza, App hii itakusaidia kuweza kusahisha makosa yote ya maneno ya kingereza pamoja na matamshi yake wakati wa kuyandika.

Na hizo ndio programu nilizo kuandalia kwa siku ya leo, Kama ulipitwa na makala iliyopita ya programu bora za kujaribu kwenye simu yako ya Android unaweza kusoma makala hiyo hapa. Kama una maswali maoni au umependa app hizi tuandikie kwenye maoni hapo chini.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use