Apps# 2 : Jaribu App Nzuri Kwenye Simu Yako ya Android

Sehemu ya 2 jaribu programu hizi mpya kwenye simu yako ya Android
App nzuri za Android App nzuri za Android

Soko la Play store limejaa programu nyingi mbalimbali, ni kweli kuwa hatuwezi kuwa tunajua programu zote zilizopo kwenye soko hilo. Lakini kwa msaada wa Tanzania Tech utaweza kupata kujua pamoja na kujaribu programu mbalimbali ambazo pengine ulikuwa huzijui kabla. Bila kupoteza muda twende tukangalie programu za leo.

1. Smart Tools : Compass, Calculator, Ruler, Bar Code

Smart tool ni moja kati ya programu nzuri sana, programu hii inakupa uwezo wa kuwa na vitu mbalimbali kwenye simu yako kama vile, tochi, rula, kikokoteo, pima maji, dira  na vifaa vingine vingi ambavyo ungependa kuwa navyo kwenye simu yako, kizuri ni kuwa Smart tools inakupa vyote hivyo ndani ya App moja huna haja ya kuinstall app nyingine.

2. VolumeSlider

VolumeSlider
Price: Free+

Endepo labda simu yako imeharibika kitufe cha kuongeza au kupunguza sauti au labda unapata kazi kuongeza sauti kwa mkono mmoja basi app hii itakuwa msaada mkubwa kwako. Kwa kutumia Volume slider utaweza kuweka sehemu ya kuongeza na kupunguza sauti kwenye pembe ya kioo cha simu yako, hivyo kila mara utakapo taka kuongeza au kupunguza sauti utagusa kwa kupapasa kwenye pembe za kioo chako na utaweza kuongeza au kupunguza sauti.

Advertisement

3. Meteor Swipe – Edge sidebar launcher

Meteor Swipe
Price: Free

Tukiendelea kubaki kwenye pembe ye kioo chako app ya Meteor Swipe hii ni tofauti na app ya Volume Slider ambayo na yenyewe inafanya kazi kwenye pembe ya kioo chako. App hii ya Meteor Swipe itakupa uwezo wa kuweka Shortcuts au njia rahisi ya kufungua programu unazo zipenda au kuzitumia mara kwa mara. Utakacho fanya ni kupapasa kidole kwa kuvuta kushot au kulia na programu unazo zipenda zitatokea kwenye upande wa kushot au wa kulia wa simu yako.

4. POLA Camera – Beauty Selfie, Clone Camera& Collage

POLA Camera ni app bora kwa wale wanaopenda sana picha, lakini unaweza kudhani app hii ni kama app nyingine za picha hapana App hii ni bora kutokana na sehemu yake ya Clone. Sehemu hii itakuruhusu kuweza kutengeneza picha zinazo fanana kwa kutumia picha moja yaani unapiga picha mtu au kitu kikiwa kwenye sehemu moja kisha una hama na kwenda sehemu nyingine kisha app hiyo itaonyesha vitu vyote vitatu ndani ya picha moja…mhh sijui kama umenielewa..hebu jaribu app hii mwenyewe utanielewa.

5. THRIVE

THRIVE AWAY
Price: Free

Tofauti na App nyingine kwenye list hii app ya THRIVE ni app inayo kusaidia kuweza kuondokana na kupata ugonjwa wa kupenda sana Smartphone, App hi inakusaidia endepo kuna wakati hutaki kabisa kukaa karibu na mitandao kwama Facebook, Instagram na mitandao mingine. App hii itazima programu hizo kwa muda fulani utakapo kuwa umeweka pia inauwezo wa kuzuia meseji na kumjibu mtu aliyekutumia kuwa kwa sasa uko mbali na simu app hii ina mambo mengi sana mazuri ijaribu sasa ujionee.

Na hizo ndio programu ambazo nadhani ni bora kwako na pengine ungependa kujaribu kwenye simu yako ya Android. Kama ulipitwa na Programu za wiki iliyopita unaweza kusoma programu hizo hapa.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use