Wote tunajua kuwa ulinzi wa Fingerprint ni moja ya ulinzi wa simu ambao ni salama zaidi kwa sasa, lakini pia tumesha zoea kuwa sehemu hii ya ulinzi wa Fingerprint huwa na kitufe maalum nyuma ya simu au hata kwenye kwenye baadhi ya simu huwa kwenye kitufe maalum mbele ya simu maarufu kama (Home Botton).
Lakini kampuni ya Vivo kupitia mkutano wa CES 2018, imekuja na simu ya kwanza duniani ambayo inayo sehemu hiyo ya fingerprint kwenye kioo cha simu.
Simu hii mpya ya Vivo inatumia sensor mpya inayoitwa Synaptics optical sensor, iliyo anza kutengenezwa miaka mingi na sasa hadi kufikia mwaka huu 2018 hii ndio simu ya kwanza inayotumia sensor hiyo kuweza kuwezesha ulinzi wa fingerprint kwenye kioo cha simu.
Jinsi sehemu hii inavyofanya kazi ni kuwa sensor ya Synaptics optical sensor inatumia nafasi (uwazi) baina ya pixel zilizoko kwenye kioo cha OLED ili kuweza kusoma alama za vidole ili kuweza kufungua simu yako. Hata hivyo bado simu hii ya Vivo haina jina kamili ikiwa ni ishara ya simu hii kutokuwa tayari kuingia sokoni.
Teknolojia hii ya kuweka fingerprint kwenye kioo inategemewa kuja kwenye simu nyingi miaka ya karibuni kutokana na senseor zenye uwezo huu kuanza kutengenezwa kwa wingi ikiwa imepewa jina la “Clear ID sensor”.
Kwa taarifa zaidi za mkutano wa Consumer Electronic Show (2018), unaweza kufuatilia ukurasa wetu maalum wa CES 2018 na utapata taarifa zote kuhusu mkutano huu pamoja na yote yatakayo jiri.