Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kampuni za Simu Kuanza Usajili wa Laini kwa Kutumia Alama za Vidole

Sasa usajili wa laini za simu kuboreshwa zaidi kwa kuongeza alama za vidole
Usaili wa Laini kwa Alama za Vidole Usaili wa Laini kwa Alama za Vidole

Hivi karibuni kampuni za simu za hapa Tanzania zita anza kufanya usajili mpya wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole au fingerprint.

Kwa mujibu wa Taarifa hizi ambazo tumezipata kupitia SMS kutoka kampuni mbalimbali za simu ni kuwa, sehemu hiyo itakuwa kuwa kama sehemu ya ziada ili kuongeza usalama zaidi wa mwenye laini. Yani pale mtu atakapo amua kusajili laini itambidi awe na kitambulisho na itabidi pia anaye sajili aweke alama zake za vidole kwa ajili ya usalama zaidi.

Advertisement

Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa kutoka kampuni mbalimbali za simu za hapa Tanzania usajili huo wa kutumia alama za vidole unategemewa kuanza rasmi tarehe 5 mwezi wa pili mwaka huu 2018 (5/2/2018) na utaratibu huu utakua ni utaratibu ambao utatumiwa na kampuni zote zinazo sajili laini kwa ajili ya huduma za simu za mkononi hapa Tanzania. Kupata taarifa zaidi tafadhali tembelea wakala wa huduma za wateja wa kampuni ya laini unayo tumia.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

9 comments
  1. Hapa sijapata ufafanuzi zaidi, ni kwa watumiaji wote waliosajiliwa au ni kwa watumiaji wapya? Au wote kwa pamoja, wa zamani na wapya ambao wanaendelea kusajiliawa??
    Naombeni mnifafanulie tafadhali.

    1. Tafadhali wasiliana na huduma kwa wateja wa laini unayo tumia au nenda kwenye ofisi zao zilizo karibu na wewe.

  2. Maoni*na iih mpaka tufike ofisi ya mtandao au iih Huduma tutapata hata kwa mawakala wa mtaani??,,,,by friston

  3. Maoni*sawa lakn je kwalio hatujapata vitamburisho vya uraia tutafanyeja,,naomba mtueleweshe

  4. Nahitaji Msaada wa kupata link ya fingerprint Tanzania Kwa huduma ya usajili wa lain, naomba unitumie message upande wa lain ya vodacom no,0746456299

  5. Kusajili laini kwa kutumia dole gumba ni sh, ngapi? Kwa maana kila mtu ana bei yake tunaomba ufafanuzi maana imekuwa biashara kubwa sana kwa wenzetu kama kuna malipo tujuwe kama ni bure nako tujuwe lakini pia mamlaka husika isimamie au itoe bei elekezi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use