Tofauti ya Processor za Simu za Dual-core, Quad-core na Octa-core

Tambua sasa tofauti iliyopo kati ya simu zenye processor za aina hizi
Processor za Dual-core, Quad-core na Octa-core Processor za Dual-core, Quad-core na Octa-core

Kwa hapa Tanzania ni wazi kuwa watu wengi sana mara nyingi wamekua wakinunua smartphone za aina mbambali bila kuangalia uwezo wa processor, hii inatokana na kutokujua umuhimu wa processor au hata kutokuwa na ujuzi wa kuweza kungalia processor za simu hizo.

Kwa leo Tanzania Tech tunakuletea makala hii ambayo ukisoma mpaka mwisho utajua jinsi ya kuangalia uwezo wa processor ya simu yako na bila kusahau tofauti iliyopo kati ya processor za aina ya Dual-core, Quad-core pamoja na Octa-core. Bila kupoteza muda twende tukangalie tofauti hii..

  • Umuhimu wa Processor kwenye Simu

Kabla ya kuanza ni vyema ujue umuhimu wa processor. Processor kwenye simu yako ni moja kati ya kifaa muhimu sana ambacho ndicho kinacho tumika kama kichwa cha simu yako au ubongo wa simu yako. Processor ndio inayotumika kufanya kazi zote zilizoko ndani ya simu yako ikiwa pamoja na kuipa uwezo simu yako kuweza kufanya kazi mbalimbali kama kutumia internet, kutumia GPS, kamera, kucheza muziki na video pamoja na mambo mengine mengi yaliyoko kwenye simu yako.

Advertisement

Kwa kawaida Processor uwekwa ndani kabisa ya sakiti ya simu yako na huwa na muonekano mdogo sana na huwa na miguu mingi sana kama ukifanikiwa kubandua processor hiyo kwenye sakiti ya simu.

Tofauti kati ya Processor za Dual-core, Quad-core na Octa-core

  • Processor za Dual-core

Processor za Dual-core hizi ni processor za simu ambazo huwa na nguvu mara mbili ya kiwango kilicho wekwa. Kwa mfano kama processor ya simu ina uwezo wa 1.2GHz alafu processor hii ikawa ni dual core basi hapa processor hii huwa na uwezo mara mbili yani itakuwa na 2.4GHz.

Processor hizi mara nyingi huwa na uwezo wa kawaida kwenye ulimwengu wa smartphone kwa mwaka huu 2018, uwezo wa simu hizi huwa wa kawaida kuanzia kwenye programu za simu husika mpaka kwenye uwezo wa RAM kwani huwa na uwezo mdogo wa RAM. Mfano wa simu zenye uwezo wa Dual Core ni pamoja na Samsung Galaxy S2, iPhone 4S, HTC Sensation XE, Samsung Galaxy Nexus, Samsung Galaxy Note 1 na nyingine nyingi. Kifupi ni kuwa processor hizi kwa sasa hutumika kwenye simu zenye uwezo mdogo.

  • Processor za Quad-core

Processor za Quad-core hizi ni processor za simu ambazo huwa na nguvu mara nne ya kiwango kilicho wekwa. Kwa kifupi ni kuwa processor za aina hii huwa zimegawanyika mara nne kwenye processor moja ambapo huweza kutoa nguvu mara nne zaidi, kwa mfano kama processor ya simu yako ina 1.2GHz lakini ni Quad-Core basi ni sawa na kusema kwa ujumla simu yako ina uwezo wa processor ya 4.8GHz.

Processor hizi mara nyingi huwa na uwezo mkubwa ukitofautisha na Dual Core, processor hizi hutumika kwenye simu nyingi za sasa na za miaka ya nyuma kidogo kuanzia mwaka 2013 mpaka mwaka huu. Mfano wa simu zenye processor za Quad-core ni Samsung Galaxy J2 Pro, Samsung Galaxy J3 Pro, Tecno i3, Samsung Galaxy J5 Prime, Apple iPhone 7 Plus, Samsung Galaxy A5 na simu nyingine nyingi.

  • Processor za Octa-core

Processor za Octa-core hizi ni processor za simu ambazo huwa na nguvu mara nane ya kiwango kilicho wekwa. Processor hizi huwa na core nane ndani ya processor moja, Kwa mfano kama processor ya simu yako ina uwezo wa 1.2GHz lakini ni Octa-core basi ni sawa na kusema simu yako inauwezo wa processor wa 9.6GHz.

Processor hizi huwa na nguvu sana na huwa kwenye simu ambazo huwa na uwezo mkubwa wa kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja, kwa mujibu wa samsung simu nyingi zenye processor za aina hii huwa na uwezo mkubwa wa kudumu na chaji zaidi kuliko processor za Quad-core pamoja na Dual- core. Mfano wa simu zenye processor za quad-core ni kama Samsung Galaxy S5, Samsung Galaxy C7 Pro, Samsung Galaxy A8 (2018), Samsung Galaxy Note 8, Samsung Galaxy S8, Samsung Galaxy J7 Pro pamoja na simu nyingine nyingi.

Jinsi ya kuangalia Aina ya Processor kabla ya Kununua Simu

Mara nyingi kama una nunua simu mpya utakuta kipeperushi chenye kuonyesha ukubwa wa processor, kama kwa sababu moja au nyingie ujakuta kipeperushi hicho au huna box la simu hiyo basi ni vyema kuingia kwenye tovuti ya GSM Arena kisha andika jina la simu yako kisha utaona sifa kamili za simu yako kisha tafuta kipengele cha PLATFORM kwenye tovuti hiyo kisha angalia mahali palipo andikwa Chipset. Pia unaweza kuingia kwenye tovuti yetu na kuandika jina la simu yako na utapata sifa zake.

Kwa kumalizia ni vyema kujua kuwa simu zina saidiwa na vitu vingi kuweza kufanya kazi inayotakiwa hivyo basi simu kuwa na processor ndogo haimanishi kuwa simu yako haina uwezo wa kutosha bali simu hiyo huwa imetofautiana uwezo na simu nyingine. Hivyo basi ni vyema ukangalia matumizi yako ndipo ujue simu yenye aina gani ya processor kutokana na tofauti nilizo bainisha hapo juu.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use