in

Samsung Yatangaza Tarehe ya Kutoka kwa Samsung Galaxy S9

Sasa jiandae kwa kamera bora na muonekano mzuri zaidi

Samsung Galaxy S9

Tayari kampuni ya Samsung imethibitisha siku ya kutoka simu kwa Samsung Galaxy S9 kwa kutangaza tarehe halisi ya uzinduzi wa simu hiyo.

Katika tangazo ambalo limetolewa na kampuni hiyo, Samsung imesema kuwa inatarajia kuzindua simu hiyo ikiwa na maboresho mpya na makubwa hasa kwa upande wa kamera. Samsung imeongeza kuwa simu hiyo itakuwa ni simu ya kizazi kipya na itakuwa na muonekano bora kuliko simu nyingine za Samsung Galaxy S.

Hata hivyo Samsung ilibainisha kuwa itazindua simu hiyo huko nchini Barcelona kwenye mkutano mkubwa wa Mobile World Congress au MWC ambao unafanyika kila mwaka kuanzia mwezi wa pili.

Kuhusu siku halisi Samsung, imesema kuwa itafanya uzinduzi wa simu hiyo siku ya jumamosi ya tarehe 25 February mwaka 2018 kuanzia mida ya saa mbili usiku (8:00 PM) kwa saa za Afrika mashariki. Unaweza kujiunga na Tanzania Tech siku hiyo kwani tutakuwa tukikuletea matangazo hayo mubashara kabisa kutoka nchini Barcelona.

Kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya Teknolojia, Pakua sasa App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia unaweza kujiunga na Channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili kujifunza mambo yote ya Teknolojia.

Zifahamu Simu Mpya za Samsung Galaxy Note 20 na Note 20 Ultra
Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.