in

Simu Nyingine ya Nokia 6 (2018) Kutoka Rasmi Ijumaa Hii

Jiandae na Simu mpya ya Nokia 6 (2018) ambayo inatarajiwa kutoka hivi karibuni

Nokia 6 (2018)

Baada ya kampuni ya HMD Global inayo simamia utengenezaji wa simu za Nokia kuzindua simu ya Nokia 6 mwaka jana 2017, Sasa kampuni hiyo inarudi tena na toleo jipya la simu hiyo la mwaka 2018.

Kwa mujibu wa tovuti ya GSM Arena, simu hiyo mpya ya Nokia 6 (2018) inategemewa kutoka rasmi siku ya ijumaa na inategemewa kuja na maboresho kadhaa. Kwa sasa habari zinasema simu hiyo itakuja na kioo cha TFT cha inch 5.5 pamoja na processor ya octa-core yenye uwezo wa 2.2GHz na 1.9GHz.

Simu hiyo pia inategemewa kuja na RAM ya ukubwa wa GB 4 tofauti na simu ya mwaka jana ambayo ilikuwa na RAM ya GB 3. Vilevile mabadiliko mengine yapo kwenye ukubwa wa ndani wa simu hiyo kwani Nokia 6 (2018) inategemewa kuja na ukubwa wa ndani wa GB 64 huku ikiwa na uwezo wa kusoma memory card yenye ukubwa wa hadi GB 128.

Mbali na simu hiyo ya Nokia 6 (2018) ambayo inategemewa kuzinduliwa nchini China, kampuni ya Nokia pia inategemea kuzindua simu nyingine mpya za Nokia 9, Nokia 8 (2018) pamoja na Nokia 3310 4G zote hizo zinasemekana kuzinduliwa mwanzoni mwa mwaka huu 2018.

Jiandae na Simu Mpya za TECNO CAMON Nchini Tanzania

Vilevile kuna tetesi Nokia inategeneza kuwa kampuni hiyo sasa inatengeneza simu mpya za Nokia 4 and Nokia 7 Plus ambazo zinategemewa kutoka ndani ya mwaka huu 2018. Kaa karibu na Tanzania Tech ili kujua yote kuhusu kampuni ya Nokia na simu inazotarajia kuzitoa.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.