in

Instagram Kuonyesha Mtu Anapokuwa Online Kupitia “DM”

Sasa utaweza kuona mtu kama yuko online kupitia sehemu ya DM

Instagram Kuonyesha Mtu Anapokuwa Online Kupitia "DM"

Instagram imeanza kutoa toleo jipya la programu zake za Android na iOS, toleo ambalo linakuja na njia mpya ya kuona mtu anapokuwa online kupitia sehemu ya Direct message au DM.

Sasa kupitia programu hizo sasa utaweza kuona mtu anapokuwa online kwa kusoma chini ya jina la mtu kama umemtumia meseji ya kupitia sehemu ya DM au Direct message.

Kwa sasa tayari toleo hilo jipya la programu ya Instagram lipo kwenye masoko yote ya Play Store kwa wanaotumia Android na App store kwa wanaotumia iOS. Unaweza kuingia kwenye soko husika kisha update application ya Instagram, kisha ingia sehemu ya DM au Direct message utaona sehemu hiyo mpya.

Vilevile kama utaki mtu aone unapokua online unaweza kuzima sehemu hiyo kupitia sehemu ya Setting kisha sogea mpaka chini utakuta sehemu iliyoandikwa Show Activity Status bofya hapo kuweka off, hapo mtu atoweza kuona kila mara unapokuwa online kupitia sehemu ya DM.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

Jaribu App Mpya ya Tanzania Tech Lite
Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.