Hivi karibuni Samsung imeanza kutuma mialiko kwa ajili ya uzinduzi wa simu yake mpya ya Samsung Galaxy S9, Lakini kabla ya kutoka kwa simu hiyo tayari tumesha fanikiwa kupata picha halisi ya muonekano wa simu hiyo mpya inayo tegemea kuzinduliwa mwishoni mwa mwezi wa pili.
Kupitia mvujishaji maarufu Evan Blass, kwenye tovuti ya VentureBeat tumefanikiwa kuweza kupata sifa kadhaa pamoja na sababu kwanini samsung imekuja na msemo wa “The Camera reimagined”.
Kwa mujibu wa tovuti hiyo ya venturebeat, Simu hizi zitakuja na uwezo wa kuchukua video za taratibu “slow motion video” kwa 480fps (frame per second) tofauti na simu za kawaida ambazo huchukua video hizo kwa 120fps au 240fps.
Lakini kitu kikubwa kwenye simu hizi ni uwezo wa Variable aperture, simu hizi zina tegemewa kuja na uwezo wa kubadilika kwa apertures kutoka f2.4 apertures hadi f1.5 apertures, kwa wale wanaojua kuhusu kamera nadhani hapa tume elewana. Lakini kama hujui chochote kuhusu kamera basi nitakujuaza angalau kidogo hapa.
Aperture kwenye kamera maana yake ni ukubwa wa kufunguliwa kwa njia ambayo mwanga huingia kwenye lensi ya kamera na kufikia sensor. Aperture hupimwa kwa f-stops, f-stops hupatikana kwa kugawanya umbali kati ya lens ilipo na ukubwa wa kufunguka kwa njia ya kuingia kwa mwanga, na kama kiasi cha f-stop ni kidogo basi ndio lens hufunguka zaidi na huruhusu mwanga zaidi na kuweza kuchukua picha nzuri. Kwa mfano angalia video hapo chini lensi inavyofunguka kwa ukubwa.
Sasa kwenye Samsung Galaxy S9 kiasi cha f-stop kinaweza kubadilika kutoka f2.4 hadi f1.5 hii kuruhusu mwanga zaidi na kumsaidia mtu kuweza kupiga picha nzuri sana hasa kwenye mwanga mdogo au wakati wa usiku. Kwa sasa kiasi cha f-stop 1.5 ndio kiasi kikubwa cha kufunguka kwa lensi cha kwanza kabisa kuwepo kwenye smartphone yoyote duniani.
Tuki achana na mambo hayo ya kamera, simu hizi mbili za Samsung Galaxy S9 na S9 Plus, zinategemewa kuja na ukubwa wa ndani wa GB 128 na RAM ya GB 6 kwa Galaxy S9 Plus na ukubwa wa GB 64 na RAM ya GB 4 kwa simu ya Galaxy S9. Simu hizi zote zinategemewa kuzinduliwa tarehe 25 february 2018 na kuanza kuwafikia watu kuanzia tarehe 16 ya mwezi March 2018.
Kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya Teknolojia, Pakua sasa App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia unaweza kujiunga na Channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili kujifunza mambo yote ya Teknolojia kwa njia ya video.