Kampuni ya SanDisk Yatangaza Flash ya (TB) Terabyte 1

Sio flash kubwa kuliko zote duniani, lakini ni flash ndogo ya TB 1

Wengi wetu tumesha zoea kuwa Terabyte 1 inakuwa kwenye Hard Disk kubwa, lakini kampuni ya SanDisk kupitia mkutano wa CES 2018 imezindua Flash yenye ukubwa wa Terabyte 1 au TB 1.

Pamoja na kuwa flash kubwa kuliko zote duniani ni flash ya TB 2 kutoka kampuni ya Kingston, lakini bado kampuni ya SanDisk wameweza kuleta flash ya TB ikiwa na umbo dogo kuliko flash ya TB 2 kutoka kampuni ya Kingston.

Tofauti na flash zingine flash hii ya SanDisk ya TB 1 inatumia USB Type C yaani inaweza kuingia hata kwenye simu yako (kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini). Hivyo sasa utaweza kuhamisha vitu kutoka kwenye simu yako mpaka kwenye kompyuta yako.

Kwasasa flash hii iko kwenye hatua za mwanzoni na bado haijatangazwa ni lini flash hii itaingia sokoni kwaajili ya wateja kuinunua. Maonyesho ya CES 2018 bado yanaendelea na kama unataka kupata habari zaidi kuhusu mkutano huu fuatilia ukurasa wa CES 2018 hapa.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

Apple Yaja na Huduma Mpya za Apple TV Plus, Apple Card na Nyingine
Amani Joseph

Imeandikwa na Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.