Jinsi ya Kutengeneza App ya Android kwa Kutumia Smartphone

Kwa kutumia njia hii utaweza kutengeneza app ya Android yenye kufanya kazi

Katika ulimwengu huu ambao simu za mkononi zinatumika kwenye kila kitu ni wazi kuwa, baadhi ya vitu sasa vinawezekana kufanyika bila kutumia kompyuta. Kwa siku ya leo tutaenda kujifunza jinsi ya kutengeneza programu za Android kwa kutumia simu yako ya mkononi.

Kwa kuanza basi ili kuweza kufanikisha hili unaitaji simu yoyote ya Android pamoja na bando angalau MB 500 au zaidi, hii ni muhimu sababu ni lazima ujaribu kila sehemu ili uweze kupata kile unacho hitaji kwenye app yako hivyo ni muhimu kuwa na bando ya kutosha.

Kama tayari una bando la kutoka basi twende tukaanze somo letu la leo, lakini awali ya hapo labda nikuonyeshe picha za programu ambayo nimetengeneza kwa kutumia simu yangu ya mkononi, unaweza kudownload app hii HAPA ili kujionea mwenyewe.

Kwa kuanza basi ingia kwenye kisakuzi cha Google chrome kisha ingia kwenye tovuti ya www.andromo.com kishanga utapelekwa kwenye ukurasa maalum, bofya kitufe chenye mistari mitatu kilichoko juu upande wa kulia kisha bofya sehemu iliyo andikwa Sign Up, baada ya hapo utaletewa fomu yenye sehemu ya kujaza, jaza fomu hiyo ili kujiunga na tovuti ya Andromo na hakikisha unatumia barua pepe (email) sahihi.

Baada ya kuhakiki barua pepe yako na kuruhusiwa kuingia kwenye tovuti hiyo, sogea chini kidogo kisha utaona sehemu imeandikwa Create New App, bofya hapo kisha chini ya Project name andika jina la App unayotaka kutengeneza kisha bofya Create.

Baada ya hatua hiyo utaletwa kwenye ukurasa unao anza na Settings kutoka upande wa kushoto, bofya hapo kisha shuka chini kidogo mpaka mahali palipo andikwa Target Market, hapa ni vyema kuwa makini sababu app hii unayo tengeneza sasa utaweza kutuma Play Store sababu mpaka sasa hii ni akaunti ya bure unayo tumia, hivyo kwenye sehemu ya Target Market ni vyema kuchagua Samsung Apps au Amazon Appstore kwani huko ndipo utaweza kutuma app yako.

Baada ya kuchagua Target Market shuka chini kidogo kwenye Category kisha chagua aina ya App ambayo unataka kutengeneza, chini yake kwenye sehemu ya Description hapa utajaza maelezo yoyote kuhusu App yako na kama huna malezo yoyote basi unaweza kuacha wazi. Baada ya kumaliza kuweka maelezo ya App yako shuka chini kidogo hadi sehemu iliyoandikwa App Icon.

Jinsi ya Kuondoa Root (Unroot) Simu Yoyote ya Android

Sehemu hii ni muhimu kwani hii ndio picha ya App yako hivyo kama tayari unayo picha ya App yako sasa ndio wakati wa kuiweka na uta bofya sehemu iliyo andikwa Choose File kisha chagua picha unayotaka ndani ya simu yako, hakikisha picha yako ina ukubwa wa 512×512 na iwe na format ya png. Baada ya kumaliza hatua hiyo shuka mpaka mwisho kabisa wa ukurasa huo kisha bofya kitufe cha Save Changes.

Kisha rudi juu kabisa mwa ukurasa kisha bofya Theme, hapo utaweza kuchangua rangi ya App yako, changua rangi zote mbili zifanane kati ya Primary Color na Accent Color, baada ya hapo shuka chini kidogo hadi sehemu iliyo andikwa Body Style chagua kati ya Material Light kupata rangi nyeupe kwenye App yako na Material Dark kupata rangi nyeusi kwenye App yako. ukisha maliza shuka mpaka mwisho wa ukurasa huo na bofya Save Changes.

Baada ya hapo rudi tena juu kabisa kisha bofya sehemu iliyo andikwa Navigation, Shuka chini kidogo hadi sehemu iliyoandikwa Title kisha andika jina la App yako kisha sehemu ya Subtitle andika msemo wa App yako kwa ufupi kwa mfano “pepsi dare for more”, baada ya hapo chini ya Upload a Header Image bofya Choose File na weka picha unayotaka ionekana juu kabisa kwenye app yako, ukimaliza shuka mpaka mwisho wa kurasa hiyo alafu bofya Save Changes.

Baada ya hapo rudi juu kabisa ya ukrasa kisha bofya Dashboard, hapa ni vizuri kuwa makini shuka mpaka sehemu iliyoandikwa Startup Mode kisha chagua Show first activity(no dashboard) kisha bofya Save Changes. Kisha kama kawaida rudi juu kisha chagua sehemu ya Activities kisha bofya sehemu ya Add an Activity kisha fuata muongozo huu.

 • About – Hapa utaweka ukurasa wa kuhusu programu yako au wewe
 • Audio Player – Hapa unaweza kuweka sehemu ya kucheza muziki
 • Contact – Hapa unaweza kuweka anwani yako
 • Custom Page – Hapa unaweza kuweka ukurasa wowote unaotaka
 • Email – Hapa unaweza kuweka barua pepe
 • Facebook – Hapa utaweza kuweka ukurasa wa facebook
 • Flickr – Hapa utaweza kuonyesha picha kutoka mtandao wa Flick
 • Google Play – Hapa utawea kuonyesha link kwenda kwenye Google Play
 • HTML Archive – Hapa unaweza kuweka ukurasa unaotumia HTML
 • Map – Hapa unaweza kuweka ramani
 • PDF – Hapa unaweza kuweka file la PDF
 • Phone – Hapa unaweza kuweka namba ya simu
 • Photo Gallery – Hapa unaweza kuweka picha mbalimbali
 • Podcast – Hapa unaweza kuweka mfumo wa Podcast
 • RSS Feed – Hapa unaweza kuweka RSS fee ya blog yako
 • SHOUTcast Radio – Hapa utaweza kuweka radio kwenye app yako
 • Twitter – Hapa unaweza kuweka ukurasa wao wa Twitter
 • Website – Hapa unaweza kuweka tovuti yako
 • YouTube – Hapa unaweza kuweka ukurasa wako wa Youtube
Jinsi ya Kubadilisha Simu Yoyote ya Android Kuwa Kama iPhone

Muongozo hua hapo juu ndio utakao kusaidia kuweza kutengeneza app yako hivyo weka vitu hivyo kulingana na app yako unavyotaka iwe, kama unataka kutengeneza app ya habari basi unaweza kutumia RSS Feed pia kama unataka kutengeneza app kwaajili ya Youtube Channel yako basi unaweza kutumia sehemu ya Youtube. Baada ya hapo malizia kwa kurudi juu kisha bofya sehemu ya Build kisha kisha chagua sehemu iliyoandikwa Build My App.

Subiri mpaka programu yako ikamilike kisha utaona email au barua pepe ambayo itakuwa na programu yako ya Android, pia kwenye ukurasa huo baada ya app kukamilika utapata sehemu ya kudownload app yako na ijaribu ili kuona kama inafanya kazi inavyotakiwa.

Somo linalofuata nitakuelekeza jinsi ya kuweka App hi kwenye soko la Samsung Store ikifuatiwa na jinsi ya kuweka App hiyo kwenye soko la Amazon Store.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Maoni 39

Toa Maoni Hapa
 1. aise pindi nimelielewa lakini ujaelezea kitu kimoja kuusu kupost kitu kwenye app ulio tengeneza naomba tuwasiliabe 0755471946

 2. Nilikua nauliza kuhusu kuandika username katika kujisajiri nimejaribu ila inakataa..
  Je unaeza npa mfano wa jina ambalo wao wanalihitaji

 3. jee naweza nikaiunganisha hiy app niliyoitengeneza kwenye blog ili posti za kutoka kwnye blog yangu ziwe zinaingia kwenye app automatically

 4. app nmetengeneza lakn ina sehemu ya about tu hamna kitu kngne sasa na kupost itakua pale kwenye activity nmekosea kuhusu kujaza maana hata sielew najaza nn

 5. Kwanza niwape pongezi kwa maelezo yeah mazuri, sema ninachotaka kujua ni kwamba!!, nitawekaje ama nitapostije mambo yang kwenye hiyo app ili mtu akiidownload aweze kuona na Haina gharama kwa upande Wa Jodi-TCRA!??

 6. broh,,, nmetengeneza app keaajiliya site ya music,,

  shida niipatayo ni wakati wa kudownload nyimbo inakubali lakin ikishadownload.. kinachotokea sio wimbo tena ni attachment/document (mfumo wa maandish )naomba kujua ni nin sababu na naisolve vp

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.