SMS Yafikisha Miaka 25 Toka Kuanzishwa Kwake Mwaka 1992

Siku ya Jana mfumo wa ujumbe mfupi wa maneno umefikisha miaka 25
Ujumbe mfupi wa Maneno SMS Ujumbe mfupi wa Maneno SMS

Hapo jana tarehe 3 december dunia iliungana pamoja ikiadhimisha teknolojia ya ujumbe mfupi wa maneno SMS kufikisha miaka 25 toka kuanzishwa kwake.

Kwa wale ambao pengine hawajui kidogo kuhusu hili ni kuwa SMS ya kwanza ilitumwa tarehe 02, December 1992 na ilitumwa kupitia mtandao wa Vodafone na mhandisi mwenye umri wa miaka 22 aliyekuwa anaitwa Neil Papworth.

Ujumbe huo mfupi ulitumwa kwa njia ya kompyuta na ulikua ukisema “Merry Christmas.” aliyepokea ujumbe huo ni mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya Vodafone kwa wakati huo ambae alikua anaitwa Richard Jarvis. Historia haijaishia hapo kwani mwaka 1993 kampuni ya Nokia kwa mara ya kwanza ili-anza kuweka sehemu ya SMS kwenye simu zake sehemu iliyokua inaruhusu SMS ya idadi ya maneno 160 tu.

Advertisement

Hadi kufikia mwaka 1999 ujumbe mfupi wa maneno SMS uliwezeshwa kwenye makampuni mbalimbali ya simu na hapo ndipo mabadiliko yalipo anzia na kufanya watu kuboresha teknolojia hiyo ya ujumbe mfupi huku nchini japan wataalam wakibuni emoji ya kwanza kabisa.

Toka miaka hiyo hadi sasa teknolojia ya ujumbe mfupi imebadilika sana, tomeona mabadiliko makubwa kuanzia SMS kuwa na idadi kubwa ya maneno hadi uwezo wa kutuma ujumbe mfupi kwa kutumia internet kupitia programu mbalimbali kama za WhatsApp na nyingine kama hizo.

Kuadhimisha miaka hii 25 ya ujumbe mfupi wa maneno SMS, tungependa kuadhimisha kwa kuwakumbusha jinsi teknolojia ilivyo na umuhimu kwani kwa sasa ukifikiria maisha bila SMS basi unaona kweli mawasiliano yangekuwa magumu sana, hivyo ni vyema kujifunza na kufuatilia teknolojia kwani ndio chanzo kikubwa cha mawasilino baina yetu.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use