in

Samsung Yazindua Kioo Kikubwa cha Kompyuta cha Inch 49

Kioo hichi ni cha kwanza kwaajili ya game chanya teknolojia ya DisplayHDR

Samsung Yazindua Kioo Kikubwa cha Kompyuta cha Inch 49

Pamoja na kuwa ni karibia na mwisho wa mwaka lakini bado kampuni ya Samsung inaendela na harakati za kutoa bidhaa bora kwa watumiaji wake.

Hivi karibuni kampuni ya Samsung imezindua kioo kikubwa cha inch 49 chenye uwezo wa QLED huko inchini india, mbali na kioo hicho kuwa kikubwa kioo hicho pia kimetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu ya HDR au High-dynamic-range imaging.

Kioo hicho ambacho kimepewa sifa ya kuwa kioo kikubwa duniani kwaajili ya Game, ni kioo cha kwanza kudhibitishwa na VESA kuwa na teknolojia ya DisplayHDR™ Certification. Kama nimekuacha kidogo VESA kirefu chake ni Video Electronics Standards Association hili ni shirika la viwango vya vioo vya kompyuta ambalo makao yake makuu yako huko marekani kwenye mji wa California.

Kioo hichi chenye model namba za QLED CHG90 kina aspect ratio ya 32:9, resolution ya 3840 x 1080, na mkunjo au curvature ya 1800R , pamoja na 144Hz refresh rate. Kioo hichi kina uzito wa lbs 33.1 sawa na kilogram 15.01391.

Makosa 4 Yanayofanya Laptop Yako Kuharibika Haraka

Kioo hichi cha Samsung QLED CHG90 kina uzwa kwa dollar za marekani $1,300 sawa na shilingi za kitanzania 2,100,000 hiyo ni kwa mujibu wa viwango vya fedha vya siku ya leo, kumbuka pia kwa Tanzania bei inaweza kubadilika kutokana na kodi.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.