in

Hizi Hapa Filamu Bora za Teknolojia za Kuangalia Christmas Hii

Angalia filamu za kiteknolojia kipindi hichi cha sikukuu za christmas na mwaka mpya

Filamu bora za teknolojia

Kwanza kwa niamba ya wapenzi na wasomaji wa Tanzania Tech napenda kutoa shukurani zangu za dhati na kuwatakia christmas njema na heri ya mwaka mpya. Na leo ili uweze kusherekea vizuri nimekuandalia filamu 10 bora za teknolojia ambazo na uhakika utafurahia kuziangalia Christmas hii.

10. Transformers The Last Night

Filamu hii ni muendelezo wa mfululizo wa filamu za Transformer ambapo inahusu viumbe kutoka nje ya dunia vilivamia dunia na kutaka kubadilisha dunia yetu kuwa dunia yao, katika viumbe hivyo kutoka nje ya dunia kuna viumbe vingine ambavyo vinataka kuisaidia dunia na kuzuia dunia isichukuliwe. Unaweza kuangalia au kudiwnload movie hii kwa kubofya hapo chini.

Download Transformers The Last Night

9. Alien: Covenant

Movie hii inahusu kundi la watu walienda kwenye sayari nyingine kuangalia kama sayari hiyo inauwezekano wa kuishi binadamu, matokeo yake walikutana na viumbe vingine ambavyo vilikua kwenye sayari kwa muda mrefu na viumbe hivyo vilianza kuwachukua mmoja baada ya mwingine.

Download Alien Covenant

8. Resident Evil The Final Chapter

Filamu hii pia ni muendelezo wa mfululizo wa filamu za Resident Evil, ambapo hadithi yake ni kuwa mwanzoni kulitokea mlipuko wa magonjwa ya ajabu ambayo yalisababishwa kwa makusudi na mmoja wa wana sayansi kwa lengo la kupunguza idadi ya watu duniani. Lakini pia wanasayansi hao walitengeneza wanajeshi wa kike ambao walikua wanafanana na hatimaye mmoja wa wanajeshi hao aliwageuka na kuungana na watu wengine kuzuia mlipuko wa virusi hivyio kuteketeza watu wote duniani.

Klabu ya Soka ya FC Barcelona Yaja na Mtandao Kama Netflix

Download Resident Evil The Final Chapter

7. Ghost in Shells

Filamu hii inahusiana na mwanadamu aliye tengenezwa kama roboti ili kupigana na mdukuaji hatari ambaye alikua anashindana na serikali kuwaonyesha watu kuhusu maovu ya serikali ya miaka ijayo.

Download Ghost in Shells

6. Kingsman: The Golden Circle

Hii ni fialmu ya Action yenye mambo ya kiteknolojia ambayo inahusiana na kijana aliyetokea maisha ya kimasikini na kinyanyasaji baada ya baba yake ku-uwawa vitani. Kijana hyo anachukuliwa na mmoja wa watu waliokuwa wanafanya kazi na baba yake na kufundishwa na hatimaye anakuwa mtu muhimu kwenye ulinzi wa taifa.

Download Kingsman The Golden Circle

5. Life

Life ni filamu ambayo inahusu teknolojia, ambapo watu kadhaa walio chaguliwa kutoka nchi mbambali walipewa kazi ya kwenda mwezini na kuchunguza viumbe vilivyomo humo. Watu hao walishangzwa kugundua kiumbe kimoja kilicho wazidi akili na kuanza kuwashambulia mmoja mmoja.

Download Life

4. Valerian and City of Thousand Planets

Kama utakuwa umengalia filamu ya Avatar basi filamu hii haina utofauti sana movie hii inahusisha watu wa sayari nyingine ambao walikua wanapambana ulimwengu wao usiharibiwe na wavamizi.

Download Valerian and the City of a Thousand Planets

3. Blade Runner 2049

Mapya Mfumo wa MacOS Big Sur, Watch OS na iPad OS

Filamu hii inachukua nafasi miaka ya mbele yaani 2049, ambapo inaelezea kuwa dunia imefikia mwisho na watu wanatengeneza watu ambao ni roboti kwaajili ya kulinda amani, Mmoja ya roboti anawageuka na kuangusha serekali iliyokuwa ina fanya unyanyasaji kwa watu.

Download Blade Runner 2049

2. Snowden

Filamu hii inahusu maisha halisi ya mfanyakazi wa zamani wa shirika la kijasusi la marekani ambalo lilikuwa lifanya upelelzi wa simu mbalimbali za watu bila watu kujua. Snowden alivujisha siri hii na sasa amekimbilia huko rusia kuomba ulinzi. Hii ni stori ya kweli.

Download Snowden

1. The Circle

Hii inahusiana na msichana mmoja aliye enda kufanya kazi kwenye kampuni moja kama vile Google na Facebook lakini kampuni hii inaitwa Circle, kampuni hii ilibuni teknolojia ambazo zilikuwa zimevuka mipaka na kunyima watu kuwa na usiri.

Download The Circle

Na hizo ndio filamu ambazo zinahusi sayansi na teknolojia ambazo naona unaweza ku-enjoy kuangali kipindi hichi cha sikukuu. Je kuna filamu zingine zipi ambazo zinahusu teknolojia ambazo unahisi zingetakuwa kuwepo kwenye list hii. Tuambie kwenye maoni hapo chini.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.