in

Sasa Utaweza Kufanya Ultra Sound kwa Kutumia Simu ya Mkononi

Kifaa kipya cha IQ kitakupa uwezo wa kufanya Ultra Sound kwa simu

iQ

Kampuni inayo chipukia ya Butterfly Network, hivi karibuni imefanya ugunduzi wa kifaa kipya kinachoitwa iQ. Kifaa hichi kinauwezo mkubwa wa kumuwezesha daktari au mtu yoyote kuweza kufanya Ultra Sound kwa kutumia simu ya mkononi maarufu kama smartphone.

Kifaa hicho kidogo cha IQ ni kama vile umebeba maabara nzima kwenye kiganja cha mkono wako kwani kifaa hicho haki hitaji mtaalamu wa kukiendesha na badala yake unachotakiwa kufanya ni kukipachika kwenye simu yako ya iPhone na moja kwa moja utaweza kuanza kufanya ultra sound mwenyewe.

Wote tunajua kuwa vifa vya kawaida vya ultra sound vinatumia teknolojia ya compressed charged crystals au ceramics kuweza kutuma sauti ambayo baadae mwagwi wa sauti hiyo unapimwa kwa kutumia picha ambayo ndio inayo onekana kwenye kifaa cha ultra sound.

Lakini kwenye kifaa cha IQ teknolojia hiyo imebadilishwa na sasa kifaa hicho kitatumia teknolojia ya capacitive micromachine ultrasound transducers au (CMUT). Ambapo kifaa hicho kinakuwa na vimistari vidogo vyanye vitufe kama ngoma ambavyo hutoa mtetemeko kulingana na eneo inapo elekezwa na mtetemeko huo baadae kupimwa kwa kutumia mfumo maalum ambao hutumia data kuweza kutengeneza picha ambayo utaweza kuiona kwenye simu yako ya mkononi.

Japokua kifaa hicho hakina uwezo wa kuonyesha picha angavu kama zile za MRI au CT scan, lakini kifaa hicho kinauwezo mkubwa wa kupima sehemu mbalimbali zile ambazo haziitaji wewe kufika kwenye maabara kubwa ya kidaktari. Kwa sasa kifaa hicho kimeruhusiwa kutumika kwa madaktari tu huku jitihada zikiendelea kuwezesha kuhakikisha kinawafikia watumiaji wote wa majumbani.

Facebook Yaja na Sehemu ya Kufuatilia COVID-19 Tanzania

Kifaa hicho kinauzwa kwa kwa makadirio ya dollar za marekani $2000 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 4,493,000 huku kampuni hiyo ikisema ni bei ndogo kwa kuweka msemo wake wa “Whole body imaging. Under $2k.” Wewe unaonaje kwenye hili..? kifaa hichi kinaweza kuwa msaada mkubwa kwa madaktari pamoja na watu wa kawaida tuambie kwenye maoni hapo chini.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia usasahau kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kupata habari zote za teknolojia kwa njia ya Video.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.