in

Sasa Twitter Inakuruhusu Kutumia Jina Lenye Idadi ya Maneno 50

Sasa utaweza kutumia jina lako kamili kama linazidi maneno 20

mtandao wa Twitter

Hivi karibuni mtandao wa twitter umekua ukifanya maboresho kadhaa, moja ya kati ya maboresho hayo ni pamoja na kuongeza idadi ya maneno kwenye tweet moja yaani kutoka idadi ya maneno 140 mpaka maneno 280.

Lakini kama haitoshi hivi karibuni Twitter imetangaza kupitia ukurasa wake kuwa sasa utaweza kutumia jina lenye idadi ya maneno 50 tofauti na awali ulikuwa unatakiwa kutumia jina lisilozidi idadi ya  maneno 20 pekee.

Hii ina maanisha sasa unaweza kutumia jina lako kamili kama limezindi herufi 20 na kuendelea. Hata hivyo hii sio kwenye upande wa username yaani hapa na maanisha lile jina unalotumia linalo anza na @, hapa na maanisha jina lako kamili. Sehemu ya @username itabaki kuwa na idadi yake ya kawaida ya maneno 15 tu.

Instagram Yaleta Sehemu ya Kutengeneza Pesa Kupitia IGTV

Twitter imeleta mabadiliko makubwa kipindi hichi cha nusu ya mwisho wa mwaka, hivi karibuni tuliona mtandao huo ukibadilisha muonekano wake pamoja na icon zake pamoja na kuongeza baadhi ya sehemu kama “night mode” sehemu ambayo inapatikana kwenye kompyuta pamoja na programu za mtandao huo.

Kuelekea mwisho wa mwaka tunategemea kuona mabadiliko mengine makubwa ya mtandao huo kwa mwaka 2018, je ungependa kuona kitu gani kikibadilika kwenye mtandao wa Twitter kwa mwaka unaofuata wa 2018..? tuambie kwenye maoni hapo chini.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia usasahau kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kupata habari zote za teknolojia kwa njia ya Video.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.