Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Mabasi ya Mwendokasi Kuongezwa Kutoka Mabasi 140 Hadi 305

Mradi huu kuweza kufikia Sinza, Masaki, Chuo Kikuu cha Dar na Maeneo ya jirani
Mabasi ya Mwendokasi Mabasi ya Mwendokasi

Hivi karibuni wakala wa mabasi yaendayo kwa kasi Dart imetengaza kuwa ina mpango wa kuongeza mabasi yake yajulikanayo kama mwendo kasi kutoka mabasi 140 yaliyopo sasa hadi kufikia mabasi 305.

Hayo yamesemwa na mtendaji mkuu wa mradi huo, Mhandisi Ronald Lwakatare wakati akiwa kwenye ziara ya siku tano na wageni kutoka nchini Rwanda ambao wamekuja kujifunza jinsi mradi huo unavyotoa huduma hapa nchini.

Advertisement

Hata hivyo mhadisi huyo alisema kuwa kuongeza mabasi hayo kutafanya wakazi wa dar es salaam kupata usafiri kwa wingi zaidi kutoka wastani wa abiria 200,000 wanao hudumiwa na mabasi hayo kwa siku hadi kufikia wastani wa abiria 400,000 au abiria 500,000. Mbali na hayo muhadisi Lwakatare alisema kuwa mradi huo unategemea kuongeza njia za mlisho kutoka mbili zinazotumika sasa hadi hadi kufikia njia tisa.

Barabara hizo zinategemewa kuwa zitawezesha usafiri kwa sehemu za Sinza, Masaki, Chuo kikuu cha Dar es salaam pamoja na maeneo ya jirani ambayo yamepaka na awamu ya kwanza ya mradi huo. Hata hivyo kiongozi huyo alibainisha yote hayo yanategemewa kufanyika pale awamu ya kwanza ya mradi huo itakapo kamilika hapo Juni mwaka 2018.

Rwanda inategemea kuanza kutoa huduma za magari ya endayo kasi kutokana na kuona kuwa ni moja ya mradi ambao umefanikiwa kwa kiasi kikubwa hapa barani Afrika. Rwanda imetuma Mamlaka ya almashauri ya jiji la Kigali huku ikiongozwa na Rwagatore Etienne pamoja na Wataalam washauri ambao ndio waliopewa usanifu wa jiji la kigali kuwezesha mfumo na miundo mbinu za  magari hayo ya mwendo kasi nchini humo.

Kwa habari zaidi za teknolojia download App ya Tanzania Tech kupitia Play Store, pia unaweza kutembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia YouTube ili kuapata habari zote kwa njia ya Video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use