Kampuni ya Simu ya TTCL Kuvunjwa na Kuundwa Kampuni Nyingine

Yapendekezwa kampuni hiyo kuwa Tanzania Telecommunication Corporation
TTCL tANZANIA TTCL tANZANIA

Kampuni ya simu  TTCL ya Tanzania ni moja kati ya zile kampuni za simu za hapa Tanzania ambazo kiukweli bado ziko kwenye wakati mgumu kutokana na utoaji wake wa huduma na mambo mengine kama hayo.

Lakini kama haitoshi hivi karibuni habari kutoka bungeni dodoma zinasema kuwa serikali iliwasilisha Muswada wa Sheria ambao unaiua rasmi Kampuni hiyo ya Simu Tanzania (TTCL) na kuanzisha shirika jipya la mawasiliano Tanzania ambalo litamilikiwa na Serikali.

Kwa mujibu wa tovuti ya TTCL hadi kufikia mwaka 2016 serikali ilikuwa ikimiliki asilimia 65 za hisa za kampuni ya TTCL na asilimia 35 zilikua zikimilikiwa na kampuni ya simu ya Bharti Airtel Tanzania BV. Lakini kufikia tarehe 23 mwezi wa sita mwaka huo huo 2016 serikali ilinununua asilimia 35 kutoka kwa kampuni hiyo na hivyo kampuni ya TTCL ilikua rasmi chini ya serikali kwa asilimia 100.

Advertisement

Aidha akiwasilisha mswada huo, Profesa Makame Mbarawa ambae ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, amesema madhumuni yake ni kuanzisha shirika hilo kwa ajili ya kulinda usalama wa nchi, kukuza uchumi na kutoa huduma kwa jamii ndani ya Tanzania bara na Zanzibar.

Katika mswada huo profesa makame amaesama, sheria hiyo mpya itaiwezesha TTCL kutekeleza majukumu yake kama shirika la umma la mawasiliano likijulikana kama (TTC) au kwa kirefu Tanzania Telecommunication Corporation.

Hata hivyo Wabunge karibu wote waliochangia kwenye mswada huo pamoja na kambi rasmi ya upinzani bungeni, walipendekeza Zanzibar ipewe nafasi mbili kati ya tano badala ya moja, ili kuleta sura halisi ya muungano. Huku Naibu Spika Dk Tulia Ackson akitahadharisha mwelekeo wa mjadala huo akisema hilo si shirika la kwanza la muungano, hivyo wasije wakaanzisha utaratibu mpya kwenye mashirika.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia usasahau kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kupata habari zote za teknolojia kwa njia ya Video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use