in

Sasa Jaribu Sehemu ya iPhone X “Animoji” Kwenye Simu ya Android

Sasa utaweza kupata muonekano unaofanana kupitia App ya Supermoji

Animoji Android

Kwa wale ambao hamfakamu kuhusu Animoji basi ni vyema kuanzia hapa, Animoji ni sehemu mpya iliyopo kwenye simu mpya ya iPhone X au iPhone 10 ambayo uruhusu mtu kuweza kubadilisha mfumo wake wa sura (facial impressions) kuwa kama sehemu ya katuni zinazotembe maarufu kama emoji.

Mpaka hapo natumaini utakuwa umepata picha angalau kidogo kuhusu Animoji, sasa basi tukirudi kwenye maujanja yetu ya siku ya leo. Hivi karibuni kumekuja programu mpya inayoitwa Supermoji, programu hii imewezesha watu wa mfumo wa Android kuweza kupata mfano wa sehemu ya Animoji kutoka kwenye iphone x.

Kama tunavyojua iPhone X inatumia mfumo wa 3D recognition system ili kuweza kufanya sehemu ya Animoji kuweza kufanya kazi kama kwenye video hapo juu, lakini wataalamu walio tengeneza App hiyo wameweza kutengeneza App hiyo inayotumia mfumo wa augmented reality system ambao ndio mfumo unaotumika kwenye programu kama Snapchat na nyingine kama hizo.

Kwenye Application hiyo utaweza kuna sehemu tatu Backgrounds, Supermoji na Effect sehemu ya bacground itakuwezesha kubadilisha muonekano wa nyuma wakati una rekodi emoji zako wakati sehemu ya Supermoji itakuwezesha kuchagua emoji mbalimbali huku Effect ikikusaidia kuongeza mbwembwe kweye picha zako za emoji maarufu kama Supermoji.

Programu za Kusaidia Kutafuta Mafile kwenye Kompyuta (Windows)

Unaweza kupata programu hii sasa kupitia Play Store kwa kubofya hapo chini na utapelekwa kwenye ukurasa maalumu wa kudownload programu hiyo moja kwa moja kwenye simu yako yenye mfumo wa Android.

Baada ya kudownload fungua App hiyo kisha bofya sehemu ya supermoji kisha chagua imoji unayotaka kisha hakikisha simu yako iko usawa na kamera ya mbele ya simu yako kisha bofya kitufe cha kurekodi ili kuanza kurekodi emoji zako zinazotembe, unaweza kubadilisha muonekano wa nyuma kupitia sehemu ya backgrounds au kuongeza mbwembwe kwenye sehemu ya Effect.

Nini maoni yako kuhusu programu hii..? unahisi inafanya kazi vizuri, tuambie kwenye maoni hapo chini. Pia usisahau kuwa, habari zote hizi unaweza kuzipata kwa urahisi kupitia App ya Tanzania Tech ambayo ipo Play Store kwa wale wenye mfumo wa Android ipakue sasa.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.