Google Yaja na App Mpya ya “Files Go” Kwaajili ya Simu za Android

Sasa ongeza uwezo wa simu yako kwa kutumia App ya Files Go
Files Go App Files Go App

Siku chache zilizopita kampuni ya Google kupitia soko la Play Store ilitoa kwa bahati mbaya na baadae kuondoa app yake mpya inayoitwa Files Go. Kwa haraka sana tayari watu mbalimbali walisha weza kupata file la App hiyo ijapokua iliondolewa kwenye soko hilo maarufu la programu za Android.

Hivi leo Makamu wa Rais wa Usimamizi wa Bidhaa wa kampuni hiyo aliandika kwenye Tweet kuwa, walipanga kuzindua App hiyo hivi karibuuni lakini baadhi ya watu tayari walisha kuwa nayo kwenye simu zao hivyo sasa wameamua kutoa App hiyo kupitia Play Store ikiwa kwenye hatua za majaribio.

Advertisement

App hiyo ya File Go imetengenezwa maalum kwaajili ya kusaidia simu yako kufuta ma-file ya sio tumika na wewe au simu yako ili kuweza kuongeza ukubwa na uwezo wa memory ya simu yako. Pamoja na hayo App hiyo inakupa uwezo wa kutuma na kupokea ma-file mbalimbali bila kutumia internet kama ilivyo sehemu ya AirDrop kwenye vifaa vya Apple.

Google inamesa kuwa App hii ni moja kati ya App zake ambazo zina lengo la kuongezea uwezo simu za Android zisizokuwa na uwezo mkubwa, App nyingine ambayo ipo ndani ya mpango huo ni App ya Youtube Go ambayo na yenyewe ipo kwenye hatua za majaribio.

Kwa sasa unaweza kupakua App ya File Go ambayo iko kwenye hatua za majaribio kwa kubofya hapo chini na utapelekwa kwenye ukurasa wa App hiyo kupitia Play Store.

Files by Google
Price: Free

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia usasahau kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kupata habari zote za teknolojia kwa njia ya Video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use