in

Google Kuzuia Watu Kuchungulia Meseji Kwenye Simu Yako

Utaweza kugundua pale mtu anapokua anachungulia meseji zako

Kuchungulia Meseji

Wote tunajua kwamba simu ya mkononi ni kifaa binafsi, lakini pamoja na hayo hii issue ya watu kuchungulia meseji za watu kwenye simu imezidi kuwa kubwa sana hasa pale mtu anapokuwa eneo lenye watu wengi ambao wamesimama au kukaa nyuma yako.

Tunakubaliana kuwa tabia hii ukosesha uhuru baadhi ya watu na kusababisha mtu kushindwa kusoma au kuandika meseji mbalimbali na kujikuta anapoteza vitu vya umuhimu kwenye maisha ya kila siku. Sasa kuliona hili watafiti kutoka kampuni ya Google wanafanya utafiti wa kuzuia mtu asiweze kuchungulia meseji zako.

Wataalamu hao kwa sasa wanafanyia majaribio ya sehemu ambayo pale unapokuwa una andika au kusoma meseji kama kuna mtu anachungulia nyuma yako basi hapo hapo kamera ya mbele ya simu yako itawaka na kumuonyesha pamoja na ujumbe kutokea kwenye simu yako kuwa kuna mtu anasoma meseji zako, angalia hapo chini majaribio ya sehemu hiyo.

Kwa kutumia mfumo wa Facial recognition wataalamu hao kutoka kampuni ya Google wameweza kufanikisha hilo huku teknolojia hiyo ikitegemea kamera ya mbele ili iweze kufanya kazi.

Klabu ya Soka ya FC Barcelona Yaja na Mtandao Kama Netflix

Kwa sasa sehemu hii ipo kwenye hatua za awali sana za ubunifu na itachukua kipindi kirefu mpaka kufikia kwenye simu yako, Wataalamu wa mambo ya teknolojia wanadai kuwa sehemu hiyo inaweza isije kabisa kwenye simu za mkononi kutokana na kuwa inabidi kamera ya mbele ya simu yako iwe imewaka saa zote kitendo ambacho kinaweza kumaliza battery ya simu yako haraka.

Lakini hata hivyo uwezekano wa sehemu hiyo kuja ikiwa inatumia teknolojia zingine ambazo azita tumia kiwango kikubwa cha battery bado ni mkubwa hivyo pengine miaka ya mbeleni hili linaweza kuja ndani ya mfumo wa uendeshaji wa simu au hata kuja kama programu ya mfumo wa iOS au Android.

Nini maoni yako kwenye hili.. Unathani hii itaweza kuzuia watu kuchungulia meseji zako hasa unapokua kwenye maeneo ya watu wengi..? tuambie kwenye maoni hapo chini. Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha umepakua App ya Tanzania Tech inayopatikana kwenye mfumo wa Android.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.