in

Video : Unataka Kununua Simu ya Google Pixel 2 Ngoja Kwanza..!

Hii ni kwa wapenzi wote wa simu mpya za Google Pixel 2

Google ni kampuni ambayo ndio yenye mfumo wa uendeshaji wa Android lakini kama haitoshi kampuni hii pia kwa sasa inayo simu zake zinazoitwa Google Pixel na kwa mwaka huu kampuni hiyo imekuja na Google Pixel 2.

Japo kuwa sijajua kama simu hii imeshafika Tanzania lakini ukweli ni kwamba baada ya kuangalia video hii nimejikuta na uamuzi mgumu sana tena baada ya Google kuweka baadhi ya vitu kwenye simu zake ambavyo nilikua nikivitaka sana.

Ukweli ni kuwa kama wewe unataka simu yenye ubora labda unastaili kuangalia video hii na kama unataka simu ambayo ni nzuri kwa sifa za ndani basi ni vyema ukanunue simu hii bila kuangalia video hii

Lakini hey ukweli ni kuwa ni vizuri uangalie video hii kwa sababu wote sisi ni watanzania na kwa matumizi ya kitanzania tunataka simu zenye ubora kutokana na maisha yetu ya kila siku.

Kifupi kwa mimi sina tatizo kabisa na simu iliyotengenezwa kwa plastik lakini ukweli sijapenda Google pixel 2 kwasababu ya Fingerprint. Kama ulivyoona kwenye video simu hiyo ikipata michubuko kwenye sehemu ya fingerprint basi sema byebye kwa ulinzi kwa njia ya alama za vidole.

Jiandae na Infinix S5 Pro Hapa Tanzania (10 April 2020)

Ukweli ni kuwa mi naona ni bora kuendelea kukaa na atlist Samsung maana simu zake nyingi zimekuwa na ubora wa hali ya juu hasa pale simu inapo pata matatizo mbalimbali yaani hata kama imepasuka kioo a.k.a (simu za kitanzania).

Hebu niambie wewe unaonaje simu hiyo ya Google Pixel 2, unadhani ni simu ambayo ungependa kuwa nayo tena kwa bei ya Tsh 1,500,000 kwa Google Pixel 2 na Tsh 1,900,000 kwa Google Pixel 2 XL..? Tuambie maoni yako hapo chini.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia usisahau unaweza kupata habari kwa haraka zaidi ukiwa na App ya Tanzania Tech. Download sasa kupitia Play Store.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Maoni 2

Toa Maoni Hapa

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.