Hatimaye tetesi za ujio wa simu mpya ya Nokia 7 sasa sio tetesi tena kwani hivi karibuni kampuni ya Nokia kupitia HMD Global imezindua rasmi simu hiyo yenye kutumia Android huko nchini china.
Simu hiyo ambayo inatoka kwanza kwa nchini china inakuja na sifa za kawaida za kioo cha inch 5.2 chenye uwezo wa kuonyesha pixel 1080p huku ikiwa na teknolojia ya IPS LCD display. Vilevile Nokia 7 inakuja na processor za Snapdragon 630 pamoja na Octa-core 2.2 GHz Cortex-A53.
Kwa upande wa RAM simu hii mpya ya Nokia 8 inakuja na RAM za aina mbili yaani RAM ya GB 4 kwenye simu yenye ukubwa wa ndani wa GB 64 na RAM ya GB 6 kwenye simu yenye ukubwa wa ndani wa GB 128.
Tukiangalia upande wa kamera simu hii inakuja na kamera ya nyuma yenye uwezo wa Megapixel 16 huku ikiwa na uwezo wa f/1.8, phase detection autofocus, Carl Zeiss optics pamoja na falsh mbili za LED (dual tone) flash. Kamera ya mbele inakuja na uwezo wa Megapixel 5 huku ikiwa na uwezo wa f/2.0, autofocus, 1.4 µm pixel size.
Simu hii inakuja na ulinzi wa finger print ambayo iko nyuma ya simu hiyo pamoja na battery isiyotoka yenye uwezo wa 3000 mAh ikiwa na uwezo wa kukaa na chaji siku moja nzima kwa kuchaji mara moja. Simu hiyo pia inakuja na teknolojia ya fast charging ambayo inawezesha simu hiyo kujaa asilimia 50 kwa nusu saa.
Simu hiyo inategemewa kuingia sokoni kuanzia tarehe 24 mwezi huu na kama kawaida ya Nokia simu zake zina anza kupatikana kwa nchi ya china na labda baadae zitaweza kupatikana sehemu nyingine. Kwa upande wa Nokia 7 simu hii itauzwa nchini china kwa Yuan ya china ¥2,499 (sawa na Tsh 850,000) kwa nokia yenye GB 64 na Yuan ¥2,699 (sawa na Tsh 915,000) kwa Nokia yenye GB 128.