in

Programu 10 Bora za Kukusaidia Kupunguza Uzito kwa Haraka

Kama unapendelea kupunguza uzito kwa haraka huu hapa msaada

App za Kupunguza Uzito

Wote tunajua kuwa uzito ukizidi ni tatizo kubwa sana lakini kuna wakati hatuwezi kuzuia kuongezeka kutokana na aina ya kazi au hata maisha yetu kwa ujumla, lakini kwa namna moja ama nyingine kama umekua ukishndwa kupunguza uzito wako basi makala hii itakusaidia.

Kwa ufupi kabisa hii ni list ya programu bora au Apps ambazo zitakusaidia kupunguza uzito na kuweka maisha yako kwenye afya inayotakiwa, ni vizuri ukitumia apps hizi uku unafanya mazoezi ambayo ni muhimu sana hasa kwenye swala zima la kujenga afya bora.

10. Calorie Counter – MyNetDiary

Hii ni moja kati ya App ambazo ni bora sana hasa kwenye swala zima la kupunguza uzito, App hii ni rahisi sana kutumia kwani inahitaji tu uweke data zako za ulaji wako, uzito wako pamoja na uzito ambao unataka kupunguza na app hii itakusaidia kukupa ushauri pamoja na kukumbusha juu ya ulaji wako.

9. Charity Miles Walk&Run Tracker

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao unapenda kusaidia wengine huku ukiweka afya yako sawa basi app hii ni bora sana. App hii inafanya kazi tofauti kidogo kwani inakupa uwezo wa kusaidia watu mbalimbali kwa kutembea yaani pale unapotembea umbali ulio tembea unageuzwa kuwa pesa ambazo zitaenda kusaidia watu mbalimbali.

8. My Diet Coach – Weight Loss

App hii itakusaidia kupunguza uzito kwa haraka kwa kuweka uzito unaotaka kuufikia na app hii itakuwa iki kukumbusha kufanya mambo mbalimbali ya kuweza kukusaidia kupunguza uzito wa mwili wako.

Apps za Kusaidia Kutuma SMS Nyingi kwa Pamoja (Android)

7. 8fit – Workouts, Meal Planner & Personal Trainer

8fit ni programu nyingine ambayo inaweza kukusaidia kupunguza uzito wako wa mwili, app hii itakupa ushauri wa aina ya mazoezi ya kufanya pamoja na uwezo wa kukupa mazoezi marahisi ambauo unaweza kufanya popote ili kupunguza uzito wa mwili wako kwa haraka.

6. Fitbit

Fitbit
Price: Free+

Fitbit ni app maarufu sana kwa kuangalia umbaili ambao unatembea huku ikikupa data mbaimbali ambazo zinaweza kukusaidia sana kuweza kupunguza uzito wa mwili wako, app hii ni moja kati ya app bora sana ijaribu sasa.

5. MyPlate Calorie Tracker

App hii ni moja kati ya app 5 bora zilizo baki kwenye list hii app hii inatengezwa na wataalamu wa afya ambao wanaendesha tovuti ya Livestrong.com tovuti maarufu kwa afya na kujenga mwili. App hii itaweza kukusaidia kuangalia chakula unacho kula pamoja na kukusisitiza unywaji wa maji ambao utakusaidia kupunguza uzito.

4. Lose It! – Calorie Counter

Hii ni app nyingine ambayo ni bora sana kwa kupunguza uzito, app hii ni moja kati ya app ambazo zinakusaidia kupunguza uzito huku unafurahia kwani app hii inakupa uwezo wa kuandika kiasi cha uzito unachotaka alafu app hii itakusaidia njia za kupunguza uzito.

Kudownload Picha na Video Kutoka Mtandao Wowote wa Kijamii

3. YAZIO – Calorie Counter

Yazio ni moja kati ya app bora sana inauwezo mkubwa sana wa kukusaidia kupunguza uzito, unachotakiwa kufanya ni kujaza baadhi ya data ambazo ni muhimu ambazo zitasaidia app hiyo kuweza kufanya kazi jinsi inavyotakiwa.

2. Calorie Counter by FatSecret

Hii ni kati ya programu ambazo zimesha saidia watu wengi sana, app hii inauwezo wa kutambua chakula kwa kutumia kamera na kuonyesha kiasi cha lishe kilichoko kwenye chakula hicho pamoja na kukupa mpangilio wa nini ule na nini usile na kwa wakati gani.

1. Calorie Counter – MyFitnessPal

Kwenye namba moja hii ni moja kati ya app zenye uwezo mkubwa sana wa kukusaidia kiafya app hii ina uwezo wa kujua aina ya chakula huku ikiwa na uwezo wa kukupa ushauri wa chakula mazoeizi pamoja na mengine mengi.

Na hizo ndio programu ambazo ukizingati ushauri unapatika kwenye app hizo basi na uhakika utaweza kupunguza uzito wako kwa haraka sana, app hizi pia zinapatikana kwenye mifumo ya iOs cha msingi ingia Apple Store kisha tafuta jina na angalia picha ya app wakati unataka kudownload ili kupata uhakika.

Kujua app zingine zinazoweza kukusaidia kwenye afya yako tembelea ukurasa huu endelea kutembelea Tanzania Tech kujua zaidi, pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka zaidi.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.