Kampuni maarufu kwa utengenezaji wa mfumo wa Windows, Microsoft hivi karibuni imetangaza kuacha utengenezaji wa simu zake zenye mfumo wa Windows 10 Mobile
Kupitia mtandao wa Twitter kiongozi msaidizi wa Windows 10 Joe Belfiore, aliandika kuwa kwa sasa kampuni hiyo haina malengo wala matarajio yoyote ya kuongeza sehemu mpya kwenye simu zenye mfumo wa Windows 10 Mobile lakini wataendelea kutoa update za kuweka ulinzi kwenye simu zilizopo sokoni.
Hivi karibuni kiongozi huyo alitangaza kuwa yeye pia ameamua kuhamia kwenye simu zenye mfumo wa Android ili kupata apps pamoja na harwera nzuri zaidi na hiyo ni baada ya muasisi wa kampuni hiyo Bill Gates naye kuhamia kwenye simu zenye mfumo huo yaani Android.
Microsoft iliacha rasmi utengenezaji wa simu zake maarufu kama Lumia hapo mwaka jana na kuacha mamilioni ya watumiaji na wapenzi wa simu hizo wakiamia kwenye mifumo ya Android pamoja na iOS.
Tuendelee kusubiri kuona nini ambacho kampuni ya Microsoft itakuja nacho kwa upande wa simu za mkononi maarufu kama smartphone.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech nasi tutakujuza yote mapya, pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka zaidi
Chanzo : BBC News