Mbunifu wa Programu Aishitaki Apple kwa Wizi wa Jina “Animoji”

Inasemekana kuwa jina Animoji alijabuniwa na Apple bali limeibiwa
Animoji na Apple Animoji na Apple

Moja kati ya sehemu zilizotangazwa na Apple kwenye uzinduzi wa iPhone 8 na iPhone X ni sehemu mpya ya Animoji. Kama ilivyotangazwa kwenye uzinduzi huo sehemu hii itakusaidia kuweza kutengeneza emoji zako binafsi zenye kutembea (Animate) pamoja na kuwa na uwezo wa kutumia emoji hizo kama meseji yenye kuongea.

Advertisement

Baada ya wiki kadhaa kupita toka sehemu hiyo ilipo tangazwa rasmi, hivi leo kumeibuka mzozo baina ya mbunifu wa programu (App Developer) na kampuni ya Apple. Mbunifu huyo aliyetambulika kwa jina la Enrique Bonansea’s anaishitaki kampuni ya Apple kwa kutumia jina la Animoji bila ya kuwa na ruhusa au kibali maalum.

Mbunifu huyo wa programu anasema kuwa alisajili jina hilo kuanzia mwaka 2014 na hadi kufikia mwaka 2015 jina hilo lilipewa ruhusa maalumu ya kutumika kama nembo ya biashara, Hata hivyo mbunifu huyo wa programu alisema kuwa Apple imetumia mabavu kuchukua jina hilo kwani ilikua inajua kabisa uwepo wa Jina hilo kupitia kwenye moja ya programu za mbunifu huyo iliyopo kwenye soko la Apple la App Store.

Programu hiyo ambayo mpaka sasa ipo kwenye soko la App Store inaonyesha kuwa imesajiliwa rasmi kwenye soko la App Store toka tarehe 30 Sep mwaka 2014. Mbali na Apple kujua uwepo wa jina hilo mbunifu huyo amesema kuwa kumekuwa na watu kadhaa pamoja na makampuni mbalimbali yalio mfuata wakitaka awauzie jina hilo.

Hata hivyo inasemekana kuwa Apple ili jaribu kutuma maombi ya kufutwa kwa jina hilo kwa upande wa mbunifu huyo siku moja kabla ya uzinduzi wa simu yake ya iPhone X, maombi hayo yalitumwa kwa madai kuwa kwa muda huo kampuni iliyofanya usajili wa jina hilo “emonster Inc.” haikua inafanya kazi rasmi.

Kwa sasa inasemekana kampuni hiyo iliyofanya usajili wa jina hilo ipo kwa jina la “emonster k.k” ambayo makazi yake yapo nchini japan baada ya mbunifu huyo kuamia nchini humo.

Kesi hiyo kwa sasa bado ipo kwenye mahakama ya U.S. District Court for the Northern District of California wakati mbunifu hyo akitaka Apple imlipe fidia kwa kutumia jina hilo kinyume na sheria.

Kwa habari zaidi za teknolojia usiache kupakua App yetu ya Tanzania Tech kupitia Play Store ili kupata habari kwa haraka zaidi.

Chanzo : Apple Inside

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use