Jinsi Hashtag ya #MeToo Inavyo Vumbua Maovu Kwenye Twitter

Wanawake waitumia kupaza sauti juu ya unyanyasaji wa Kingono
#MeToo #MeToo

Twitter ni mtandao wa kijamii unaotumiwa sana na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wakumbwa wa ndani na nje ya Tanzania kufikisha mawazo na hisia zao mbalimbali. Lakini pia mtandao huu hivi karibuni umeanza kutumika kwenye harakati mbalimbali.

Moja ya harakati ambazo zimeshika chati kwa sasa ni hashtag ya #MeToo, Hashtag hiyo ambayo imeanzishwa na nyota wa filamu wa nchini marekani Alyssa Milano, inatumika sana sasa kuwataka wanawake ambao wamenyanyaswa kingono kujitokeza na kuungana kwa pamoja.

Hashtag hiyo kwa sasa imesha ibua kesi mbalimba ikiwa pamoja na wasani wakubwa wa inchini marekani pia kujitokeza na kusema kuwa nao pia walishawahi kunyanyaswa kingono, wasanii hao ni kama Lady Gaga, Evan Rachel Wood na wengine wengi.

Advertisement

Hashtag hiyo ya #MeToo kwa sasa ni maarufu sana kwa nchi za Uingereza, Marekani, India pamoja na Pakistan. Unaweza kusoma mlolongo wa Tweet mbalimbali zenye hashtag hiyo kwa kubofya HAPA.

Je nini maoni yako unaonaje hili..? tujulishe kwenye maoni hapo chini bila kusahau unaweza kupata habari zote za Teknolojia kwa kupakua App ya Tanzania Tech kupitia kifaa chako chenye mfumo wa Android, bofya link iliyokolea rangi hapo juu kudownload au tafuta kwenye Play Store “Tanzania Tech”.

Chanzo : Quartz

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use