Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Hapa Sifa za Huawei Mate 10 na Huawei Mate 10 Pro

Huawei kurudi tena na simu zenye uwezo mkubwa na kioo cha Fullview
Sifa Huawei Mate 10 Sifa Huawei Mate 10

Hivi leo mda mchache ulio pita kampuni ya nchini china Huawei imezindua simu zake mpya za Huawei Mate 10 na Huawei Mate 10 Pro na kama kawaida yetu sasa ni muda wa kuangalia sifa za simu hizi ambazo zimetengenezwa na teknolojia mpya ya hali ya Juu.

Kabla ya kuanza ni vyema tuzifahamu kidogo simu hizi za Huawei Mate 10 pamoja na Huawei Mate 10 Pro.

Advertisement

Huawei Mate 10 pamoja na Huawei Mate 10 pro ni simu ambazo hazina utofauti mkubwa kwa macho ya kawaida lakini tukiingia kwenye sifa za simu hizi ni tofauti kabisa.

Sifa za Huawei Mate 10

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.9 chenye FullView LCD na 3D glass, 2560 x 1440 resolution
  • Uwezo wa Mtandao – 2G/3G/4G yenye kuingia line mbili moja ndio yenye 4G
  • Uwezo wa Processor – Processor mpya za Huawei Kirin 970 Octa-core CPU (4 Cortex A73 2.36 GHz + 4 Cortex A53 1.8 GHz) + i7 co-processor
  • Ukubwa wa RAM – GB 4
  • Ukubwa wa Ndani – GB 64 yenye uwezo wa kuweka Memory Card Mpaka GB 256
  • Kamera ya Nyuma – Ziko Mbili moja inayo Megapixel 20 Monochrome pamoja na nyingine yenye Megapixel 12. zote kwa pamoja zina teknolojia ya RGB sensors f/1.6, OIS , BSI CMOS, flash mbili za LED, PDAF+CAF+Laser+Depth auto focus, 2x Hybrid Zoom, pamoja na uwezo wa kuchukua video za 4K.
  • Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye f/2.0 aperture, fixed focus
  • Uwezo wa Battery – 4,000 mAh battery ambayo haitoki yenye teknolojia ya Huawei SuperCharge (simu inapata chaji asilimia 50 kwa dakika 30). Uwezo wa Battery Kudumu na Chaji ni hadi masaa 48 (inategemea matumizi)
  • Viunganishi – Wi-Fi 2.4 G, 802.11a/b/g/n/ac with Wi-Fi Direct support Tundu la headphone 3.5
  • Uwezo wa Bluetooth – 4.2, support BLE support aptX/aptX HD and LDAC HD Audio
  • Aina ya USB – Type-C DisplayPort 1.2
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8 OREO yenye mfumo wa Huawei EMUI 8.0
  • Uzito wa simu  – 186 g
  • Uwezo wa Kuzuia Maji – Haina
  • Ulinzi – Finger Print kwenye kitufe cha Home
  • Rangi – Mocha Brown, Black, Champagne Gold, Pink Gold

Sifa za Huawei Mate 10 Pro

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.0 chenye FullView LCD na 3D glass, 2560 x 1440 resolution
  • Uwezo wa Mtandao – 2G/3G/4G yenye kuingia line mbili moja ndio yenye 4G
  • Uwezo wa Processor – Processor mpya za Huawei Kirin 970 Octa-core CPU (4 Cortex A73 2.36 GHz + 4 Cortex A53 1.8 GHz) + i7 co-processor
  • Ukubwa wa RAM – GB 4 na GB 6
  • Ukubwa wa Ndani – GB 64 au GB 128 yenye uwezo wa kuweka Memory Card Mpaka GB 256
  • Kamera ya Nyuma – Ziko Mbili moja inayo Megapixel 20 Monochrome pamoja na nyingine yenye Megapixel 12. zote kwa pamoja zina teknolojia ya RGB sensors f/1.6, OIS , BSI CMOS, flash mbili za LED, PDAF+CAF+Laser+Depth auto focus, 2x Hybrid Zoom, pamoja na uwezo wa kuchukua video za 4K.
  • Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye f/2.0 aperture, fixed focus
  • Uwezo wa Battery – 4,000 mAh battery ambayo haitoki yenye teknolojia ya Huawei SuperCharge (simu inapata chaji asilimia 50 kwa dakika 30). Uwezo wa Battery Kudumu na Chaji ni hadi masaa 48 (inategemea matumizi)
  • Viunganishi – Wi-Fi 2.4 G, 802.11a/b/g/n/ac with Wi-Fi Direct support, Haina tundu la headphone inatumia USB Type C.
  • Uwezo wa Bluetooth – 4.2, support BLE support aptX/aptX HD and LDAC HD Audio
  • Aina ya USB – Type-C DisplayPort 1.2
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8 OREO yenye mfumo wa Huawei EMUI 8.0
  • Uzito wa simu  – 178 g
  • Uwezo wa Kuzuia Maji – Inayo Uwezo wa Kuzuia maji IP67 water-resistance
  • Ulinzi – Finger Print kwa Nyuma
  • Rangi – Midnight Blue, Titanium Gray, Mocha Brown, Pink Gold

Simu hizi zinakuja na teknolojia mpya na zimetengezwa na mfumo wa AI (Artificial Intelligence) ambapo kamera za simu hizi zinauwezo mkubwa wa kujua ni picha gani unayochukua. Kwa mfano kama unapiga picha chakula basi kamera za simu hizi zinaweza kujua ni chakula na kufanya marekebisho ya rangi ili picha yako ionekane vizuri.

Vilevile simu hii hizi zinakuja na uwezo wa kutumiaka kwenye kioo kikubwa kama tulivyo ona kwenye simu za samsung. Unaweza kutumia simu hii kama kompyuta kwa kuichomeka kwenye kioo na utaweza kuitumia kama kompyuta.

Mbali na hayo simu hii pia inakuja na toleo la ziada ambalo linaitwa Huawei Mate 10 Porsche design simu hiyo utofauti wake ni ukubwa wa ndani ambayo inakuja na uwezo wa GB 256.

Na hizo ndio sifa za Huawei Mate 10 pamoja na Huawei Mate 10 Pro ambazo zimetoka rasmi leo simu hizi zinategemewa kuingia sokoni hivi karibuni. Kuhusu bei mpaka sasa kampuni ya Huawei haijatangaza bei ya simu hizi lakini inategea kutangaza hivi karibuni.

Kwa habari zaidi za Teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech nasi tutakujuza yote mapya kwa upande wa teknolojia, pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote kwa haraka zaidi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use