Kwa wale wasio jua WhatsApp ya Biashara ni App mpya kutoka WhatsApp ambayo lengo lake ni kusaidia wafanya biashara mbalimbali ambapo sasa wataweza kutenganisha matumizi ya WhatsApp kwaajili ya biashara na WhatsApp kwaajili ya matumizi binafsi.
Kwa sasa App hiyo iko kwenye hatua za mwisho na tayari imesha anza kufanyiwa majaribio mbalimbali na sasa kwa mara ya kwanza hapa Tanzania Tech tumeweza kupata muonekano wa programu hiyo mpya pamoja na jinsi itakavyofanya kazi.
Kwa kuanza WhatsApp ya biashara iko tofauti kabisa na WhatsApp ya kawaida WhatsApp ya biashara ina muonekano mpya kabisa kuanzia icon yake mpaka muundo wa ndani wa programu hiyo. Programu hiyo kwasasa inayo icon yenye B katikati kama inavyonekana kwenye picha na ni App tofauti kabisa na App ya kawaida ya WhatsApp.
Muonekano wa Icon ya Programu ya #WhatsApp ya Biashara Inayokuja hivi karibuni, Kujua zaidi tembelea @tanzaniatech pic.twitter.com/gnRwTdiMs9
— Tanzania Tech (@tanzaniatech) October 11, 2017
Programu hiyo kwa sasa inajaribiwa na baadhi ya watu kutoka nchi mbalimbali ambao watu hao wanapewa ruhusu maalum ya kushiriki kwenye majaribio ya programu hiyo, kutoka kwa watu mbalimbali ambao wamejaribu programu hiyo mpya hivi ndivyo programu hiyo ilivyo kwa ndani.
Muonekano wa Ndani wa Programu mpya ya #WhatsApp ya Biashara ambayo ipo kwenye majaribio ya mwisho. Kujua zaidi tembelea @tanzaniatech pic.twitter.com/eHEpk5suuE
— Tanzania Tech (@tanzaniatech) October 11, 2017
Kwa muonekano wa programu hiyo programu hiyo itakupa uwezo wa kuona data mbalimbali kupitia sehemu mpya ya “Statics” ambapo utaweza kupata idadi ya meseji zilizo tumwa, idadi ya meseji ulizo pokea, pamoja na idadi ya meseji ulizo soma.
Kwenye #WhatApp ya biashara utaweza kupata data maalum kupitia sehemu ya Statics ambayo itakupa uwezo wa kujua jinsi ulivyotumia programu. pic.twitter.com/Ojjdc5PJgM
— Tanzania Tech (@tanzaniatech) October 11, 2017
Pamoja na hayo kwenye programu hiyo utaweza kuongeza data maalum kwenye profile yako, tofauti kabisa na ilivyo kwenye programu ya whatsapp ya kawaida. Hapo utaweza kuweka link ya tovuti yako, barua pepe, eneo biashara yako ilipo kwenye ramani, aina ya biashara pamoja na maelzo maalum ya biashara yako.
Muonekano wa Profile kwenye #WhatsApp ya kibiashara inayokuja hivi karibuni zaidi tembelea @tanzaniatech pic.twitter.com/gKjYYbvCKK
— Tanzania Tech (@tanzaniatech) October 11, 2017
Kwa kumalizia, programu hiyo mpya ya Whatsapp ya biashara inakuja na uwezo wa kuhakikiwa kwa profile kama ilivyo kwenye Facebook na Instagram, mtumiaji ataweza kuhakiki namba yake moja kwa moja kupitia app hiyo na namba hiyo itawekewa tiki ya kijani kuonyesha kuwa hiyo ndio namba halisi ya simu ya biashara yako.
Kama biashara yako itakuwa haija hakikiwa neno “Unverified Business” litakuwa chini ya jina la biashara kwenye profile yako ya WhatsApp ya biashara. Pia unaweza kutumia programu hiyo kwenye simu yako hiyo hiyo yenye WhatsApp yako ya kawaida lakini namba ndio lazima ziwe tofauti na namba inayotumika kwenye WhatsApp ya kawaida.
Kingine kizuri ni kuwa kupita App hiyo utaweza kuseti muda maalum ambao uta amua kupokea ujumbe yani kama hutaki kupokea ujumbe kwenye programu yako ya WhatsApp ya Biashara baada ya masaa ya kazi kuisha basi utaweza kufanya hivyo kupitia sehemu ya “Away Message” ambapo mtumiaji ataweza kupata ujumbe mfupi ulio weka wakati ambao sio muda wa kazi.
Kupitia #Whatsapp ya biashara utaweza kuchagua muda wa kazi ambao utapenda kupokea meseji, muda usio wa kazi mteja atapata ujumbe maalum. pic.twitter.com/s8zPtgCrbT
— Tanzania Tech (@tanzaniatech) October 11, 2017
Kwa sasa tayari programu hiyo iko kwenye soko la Play Store lakini, kwa hapa Tanzania bado hatujaruhusiwa kuweza kuijaribu. Labda kwa siku zinazokuja tunaweza kuruhusiwa kujaribu programu hiyo unaweza kubofya link hapo chini kuendelea kuangalia kama tayari Tanzania imeruhusiwa kujaribu programu hii mpya ya WhatsApp ya Biashara.
Pia unaweza kufanya maujanja mbalimbali kama unayo namba ambayo ni ya nje ya nchi basi unaweza kudownload file la APK kisha weka namba ya nchi inayoruhusiwa kujaribu programu hiyo kama vile India kisha malizia ujasili. Unaweza kudownload WhatsApp ya Biashara Apk File hapo chini.
Kwa habari zaidi za programu hii mpya na kujua lini itatoka rasmi endelea kutembelea Tanzania Tech nasi tutakujuza yote mapya, pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka zaidi.