FB Yafanya Majaribio ya Kufungua Akaunti kwa Kutambua Uso

Sasa utaweza kurudisha akaunti yako iliyofungwa kwa kutumia uso wako
Facebook-face-recognition Facebook-face-recognition

Hivi karibuni mtandao wa facebook umeripotiwa kuanza kufanya majaribio ya kufungua akaunti ya Facebook iliyofungwa kwa kutumia uso au (facial recognition).

Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali sehemu hiyo itakuwa inafanya kazi kama akaunti yako imefungwa kutokana na sababu mbalimbali za kiulinzi na itakuwa ni moja kati ya sehemu ambazo zipo sasa kama zile za kumtambua rafiki yako wa karibu na ile ya kutumia ujumbe mfupi.

Hata hivyo facebook imeongeza sehemu hiyo kutokana na sehemu zilipo awali kutokufanya kazi kwa asilimia 100, huku baadhi ya watu wakishdwa kutambua majina ya marafiki kwenye mtandao huo ikiwa ni moja ya njia ambazo facebook huzitumia kuweza kufungua akaunti yako pale inapo fungwa kutokana na sababu za kiulinzi.

Advertisement

Kwa mujibu wa tweet ya muandishi wa habari za teknolojia kutokea tovuti ya The Next Web Matt Navarra, sehemu hiyo itaonekana kama hivyo na itakuwa ikifanya kazi kwenye vifaa vyenye kamera na inategemewa kufanyia utafiti mkubwa kabla ya kuzinduliwa rasmi.

Bado haija julikana lini sehemu hiyo itakuwa tayari lakini, kujua zaidi endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka zaidi.

Chanzo : Engadget

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use