in

Mambo Unayotakiwa Kujua Kuhusu iPhone 8 Kabla ya Kuzinduliwa

Wewe ni mpenzi wa simu za iPhone, Basi haya ni muhimu kuyajua

Lile joto la uzinduzi wa simu mpya ya iPhone 8, sasa limepanda na kufikia juu zaidi kwani kwa wale wapenzi wa simu hizo kutoka kampuni ya Apple kesho wataenda kushudia rasmi simu hiyo mpya ya iPhone 8 ikiwa na muonekano mpya pamoja na uwezo wa kipekee.

Lakini kabla ya kuangalia uzinduzi wa simu hiyo basi ni vyema kufahamu haya machache kuhusu simu hiyo mpya ambayo inategemewa kutoka rasmi hapo kesho.

  • Uzinduzi wa IPhone 8 Utafanyika Kwenye Jengo Jipya la Apple

Hapo kesho Apple kwa mara ya kwanza itafungua milango ya jengo lake jipya kabisa la Apple Park ambalo lipo huko Cupertino nchini marekani. Jengo hilo ambalo kwa sasa asilimia kubwa limekamilika ni moja kati ya majengo ya kifahari na ya kipekee nchini marekani. Aidha taarifa zinasema kuwa uzinduzi wa iPhone 8 utafanyika kwenye kumbi zilizopewa jina la “Steve Jobs Theater” zinazopatikana ndani ya jengo hilo, tizama jengo lenyewe hapa chini.

  • Apple Inatarajia Kuzindua Matoleo Matatu ya iPhone 8

Kwa kawaida Apple huzindua matoleo mawili ya simu zake mpya yaani toleo la kawaida na lile toleo la “Plus” kama ambavyo tumeona kwenye iPhone 7, 6, pamoja na 5, Lakini sasa habari zinasema kuwa Apple wanatarajia kuvunja utraratibu huo mwaka huu kwa kuzindua iPhone 8 za aina tatu. Matoleo hayo yatakuwa iPhone 8, iPhone 8 Plus pamoja na iPhone X ambayo ndio ingizo jipya mwaka huu.

  • Apple Kuongeza Uwezo wa Apple Watch Kuwa na 4G / LTE
Video : Ugumu na Ubora wa Samsung Galaxy Z Flip

Kama ilivyo kawaida ya Apple, kwenye uzinduzi huo utakao fanyika kesho tegemea kuona saa mpya za Apple Watch lakini hivi sasa Apple ina-tegemewa kuongeza uwezo wa 4G/LTE kwenye saa hizo ili kukupa uwezo wa kutumia saa yako bila hata kuunganisha data kutoka kwenye simu. Vilevile Apple inategea kutoa saa hizo zikiwa zimeboreshwa zaidi ikiwa pamoja na kwenye upande wa Battery.

  • Apple Kuweka Uwezo wa Kufungua Simu yako kwa Kutambua Uso

Kama ulikua ujajua basi, ni vyema sasa ukafahamu kuwa Apple inatarajia kuweka sehemu ya kufungua simu yako kwa kutambua uso wako yaani “Facial Recognition”, kwa mujibu wa taarifa mbalimbali sehemu hiyo inategemewa kuitwa “Face ID” na mtumiaji ataweza kufungua simu yake kwa kuangalia kamera ya mbele na hapo hapo simu yako itaweza kufunguka.

  • iPhone 8 Haina Pembe za Pembeni (Bezel-less) Kama Galaxy S8

Simu mpya ya iphone 8 inategemewa kuja ikiwa haina makava ya pembeni na inategemewa kuwa nyembamba zaidi huku ikiwa na kioo kilicho boreshwa zaidi, kwa mujibu wa tetesi za mitandao mbalimbali iphone 8 inatarajiwa kuja na kioo cha OLED na sio LCD kama ilivyo zoeleka.

  • iPhone 8 Itakuwa Haina Kibonyezo cha Katikati au Home Button

Tetesi zinasema kutokana na iPhone 8 kuja ikiwa na kioo kikubwa na kava lisilo na ukiongo mkubwa basi kibonyezo cha katikati kitaondolewa na kuwekwa chini ya kioo, hii inamaanisha sasa utabonya sehemu maalumu kwenye kioo ambayo ndio itakuwa ikifanya kazi kama kitufe cha Home. (Ingawa bado hizi zinasemekana kuwa ni Tetesi).

  • iPhone 8 na Uwezo wa Kutumia Chaji Isiyo na Waya (Wireless Charge) 
Mambo Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya Infinix S5 Pro

Mbali na maboresho mengine iPhone 8 inatarajiwa kuja ikiwa na uwezo wa kutumia chaji isiyo na waya yaani Wireless Charge, sehemu hii inatarajiwa kuwa bora na iliyotengenezwa kwa teknolojia ya hali ya Juu.

  • Bei ya iPhone 8 Kuwa Ghali Zaidi Kuliko iPhone Zote

Na kwa kumalizia basi ni vyema ukajua kuhusu bei kwani mabaoresho yote hayo pamoja na sehemu mpya za simu hiyo zinakuja kwa bei ghali zaidi. Tetesi zinasema kuwa mwaka huu iPhone 8 inategemewa kuuzwa mpaka dollar za marekani $1000 ambazoni sawa na shilingi za kitanzania Tsh 2,250,000.00 kumbuka bei hii inaweza kuongezeka kwa hapa Tanzania.

Na hayondio machache niliyo kuandalia kuhusu simu mpya ya iPhone 8 ambayo itakuwa inatoka rasmi hapo kesho, kama utakuwa unataka kujua zaidi basi tungane hapo kesho mubashara kabisa tutakuletea Live kabisa uzinduzi wa simu hiyo utakao kuwa unafanyika huko nchini marekani.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa Video.

Chanzo : Technology Personalised

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Maoni 4

Toa Maoni Hapa

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.