in

Video : Tazama Ugumu na Ubora wa Simu Mpya ya iPhone 8

Wewe ni mpenzi wa iPhone 8, Basi angalia hii kabla ya kuinunua simu hii

iPhone 8

Hivi karibuni kampuni ya Apple imezindua simu mpya ya iPhone 8, simu hiyo ambayo kwa muundo haina tofauti sana na iPhone 7, sasa tayari imeshaingia kwenye majaribio mbalimbali na kwa kuanza karibu ujiunge nami kuangali ubora wa simu hii ukipitia majaribio mbalimbali.

Kwa mujibu wa video hiyo hapo juu, ubora wa iPhone 8 ni mkubwa sana ukianzia kioo hadi kava la nyuma ambalo sasa limetengenezwa kwa kioo pamoja na pembe za pembeni ambazo zime tengenezwa kwa teknolojia ya kisasa kuakikisha simu yako inadumu hasa pale inapo anguka.

Lakini pamoja na hayo kwa mujibu wa video hapo juu, iPhone 8 inaonekana kuwa na tatizo kwenye kioo chake cha kamera au lens ambacho kinaonekana kuchubuka kirahisi huku pia kinaokana kuwa juu zaidi hivyo kusababisha kuchubuka kirahisi.

Mbali na hapo simu hii inaonekana ni ya ubora wa hali ya juu sana pamoja na utengenezaji wake wenye viwango vya hali ya juu. Kwa ushayri tu ni vyema utakapo nunua simu hii uweke screen protector pamoja na kava lenye uwezo wa kufunika simu yako vizuri ili kuilinda na michubuko na mikwaruzo hasa kwenye kioo cha kamera ya nyuma.

Video : Ugumu na Ubora wa Samsung Galaxy Note 20 Ultra

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa Video.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.