Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Zijue kwa Undani Hizi Hapa Ndio Sifa za iPhone X au iPhone 10

Zitambue hizi ndio sifa kamili za iphone x
Sifa za iPhone x Sifa za iPhone x

Kampuni ya Apple leo ilitoa toleo jipya kabisa la iPhone X au iPhone 10, simu hii ambayo ina mabadiliko makubwa ya muonekano pamoja na maboresho mapya kabisa kwenye simu za iPhone.

Advertisement

iPhone X inakuja na maboresho mapya hasa kwenye uwezo wa kufungua simu hiyo kwa kutambua uso kwa kutumia sehemu ya Face ID pamoja na uwezo wa kutengeneza emoji zinazo cheza kwa kutumia sehemu ya Aniemoji, sifa zingine za simu hiyo ni kama zifuatazo.

Sifa za iPhone X au iPhone 10

  • Ukubwa wa Simu – 143.6mm x 70.9 x 7.7 mm
  • Uzito wa Simu – 174g
  • Ukubwa wa Kioo – inch 5.8 yenye teknolojia ya OLED True Tone display pamoja na resolution ya 2436 x 1125 resolution at 458 ppi, 625cd/m2 brightness, and 1,000,000:1 contrast ratio (Super Retina display)
  • Uwezo wa Processor – six-core A11 Bionic chip with 64-bit architecture, neural engine, and M11 motion coprocessor
  • Ukubwa wa RAM – GB 3 (haijadhibitishwa)
  • Ukubwa wa Ndani – Zipo Aina Mbili GB 64 na GB 256
  • Kamera za Nyuma – Zipo mbili zenye uwezo wa megapixel 12 wide-angle camera yenye f/1.8 aperture na nyingine yenye Megapixel 12 f/1.8 camera yenye f/2.8 aperture, optical zoom up to 2x, optical image stabilizatio
  • Kamera ya Mbele – Megapixel 7 yenye FaceTime camera with f/2.2 aperture
  • Ulinzi – TrueDepth camera for Face ID 3D facial recognition
  • Uwezo wa Wi-Fi – 802.11a/b/g/n/ac Wi‑Fi with MIMO
  • Uwezo wa Mtandao – LTE Advanced
  • Uwezo wa Bluetooth – Inatumia teknolojia ya Bluetooth 5.0
  • Mfumo wa Uendeshaji – iOS 11
  • Uwezo wa Kuzuia Kuinga Maji – IP67 splash, water, and dust resistance
  • Uwezo wa Battery – Inakaa hadi masaa 14 (ukiwa unaongea), Masaa 12 (ukiwa unatumia Internet), Masaaa 13 (ukiwa unangalia video) pamoja na Masaa 40 (ukiwa unasikiliza mziki)
  • Uwezo wa Chaji – inauwezo wa fast-charging inaweza kujaa chaji asilimia 50 ndani ya dakika 30.
  • Uwezo wa Kuchaji Bila Waya – Inauwezo wa Kuchaji bila waya huku ikiwa na teknolojia ya Qi wireless charging support
  • Bei – Dollar za Marekani $999 sawa na Tsh 2,250,000 (Bei inaweza kuongezeka kwa Tanzania)

Na hizo ndio sifa za iPhone X au iPhone 10 ambayo imezinduliwa hivi leo, simu hii pia itanza kupatikana rasmi kuanzi mwezi November na kwa Tanzania tunaweza kuipata kuanzia mwezi wa January au Mwishoni mwa mwaka huu 2017. Pia unaweza kusoma hapa sifa za iPhone 8 pamoja na iPhone 8 Plus.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa Video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use