in

Jiandae na Simu Mpya iPhone 8 Tarehe 12 Mwezi Huu September

Simu mpya ya iPhone 8 kuja mwezi huu september

Habari zilizo dhibitishwa kutoka kampuni ya Apple zinasema kuwa simu mpya ya iPhone 8 ina tarajiwa kutoka mwezi huu. Habari kutoka kwenye tovuti ya thenextweb zinasema kuwa mbali na iPhone 8 Apple inatarajia kuzindua bidhaa zingine mpya.

Ikiwa tayari kampuni ya Apple imesha tuma mialiko mbalimbali kwa vyombo vya habari iphone 8 inatarajiwa kuja rasmi siku ya tarehe 12 ambapo simu hiyo inategemewa kuja na maboresho makubwa sana ikiwa pamoja na muonekano mpya.

Tayari mambo mengi yamesha semwa kuhusu simu hii lakini itakubidi kusubiri tarehe 12 ili uweze kudhibitisha hayo, kwa sasa inasemekana simu hiyo inaweza kuuzwa kwa gharama kubwa sana mpaka dollar za marekani $1000..duh

Tusubiri tuone mpaka hapo tarehe 12 simu hiyo itakapo toka na kujua zaidi kuhusu tetesi za simu hiyo unaweza kusoma hapa kupitia Tanzania Tech.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa Video.

Hizi Hapa Simu za Infinix za Bei Rahisi kwa Mwaka (2020)

Chanzo : The Next Web

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.