Wakati zimepita siku chache toka kuzinduliwa kwa simu za iPhone 8, iPhone 8 Plus pamoja na iPhone X, hivi leo kampuni ya Google nayo imetangaza kuja na toleo jipya la simu zake za Pixel maarufu kama Google Pixel ifikapo October 4.
Kampuni hiyo imethibitisha hilo kwa kuweka matangazo mbalimbali kwenye mtandao wa Youtube pamoja na kwenye matangazo ya barabarani maarufu kama billboard huko nchini marekani.
Google pixel ni moja kati ya simu zenye ubora sana kwenye upande wa mfumo wa uendeshaji na mwaka huu Google inatazamia kuongeza ubora zaidi kwa kuweka ubora wa battery pamoja na mambo mengine mbalimbali.
Aidha katika tetesi za mtandaoni, wataalamu wa mambo ya teknolojia wanasema simu hiyo itakuja na processor mpya ya Snapdragon 835 huku ikisaidiwa na RAM kubwa ya GB 4 pamoja na ububwa wa ndani unao anzia GB 64 hadi GB 128.
Kwa sasa bado hakuna habari zaidi za kuvuja kwa picha za simu hiyo lakini pengine tutegemee hayo kuanzia siku za karibuni, endelea kutembelea Tanzania Tech kupata habari zaidi za simu hii mpya kutoka kampuni yenye umiliki wa mfumo wa Android.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa Video.
Chanzo : The Next Web
Nazisubiri kwa hamu sana hizi simu
Karibuni sana Msinam
iko poa sana blog hii daah
Karibu sana