Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

DIT na Veta Kuanzisha Kozi Kwajili ya Mafundi Simu Tanzania

Sasa mafundi simu wa Tanzania kusomea kazi ya ufundi simu
Fundi simu Fundi simu

Ufundi simu ni moja kati ya kazi ambazo zinachukuliwa kuwa sio rasmi sana hii ikiwa na maana kuwa mtu yeyote anaweza kufanya kazi hizi. Lakini yote hayo yanaenda kubadilika kwa siku za karibuni.

Mabadiliko hayo ambayo yataletwa na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam au (DIT) pamoja na Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) yamelenga kuanzisha mtaala wa mafunzo kwa ajili ya mafundi simu nchini baada ya kubaini wengi wao kutokuwa na elimu hiyo na kuisababisha sekta ya mawasiliano kukabiliwa na changamoto.

Advertisement

Akifungua mkutano uliowakutanisha mafundi simu jijini Dar es salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Fortunata Mdachi, amesema waliwaomba DIT na VETA kufanya utafiti na kubaini kwamba kuna uhitaji mkubwa kiasi gani wa ujuzi katika sekta hiyo na wameona kuwa kuna sababu ya kuwepo kwa vigezo vitakavyo muwezesha fundi wa simu kufanya kazi hiyo kwa uhakika.

Akinukuliwa na gazeti la mwananchi Mkurugenzi huyo alisema, “Teknolojia ya simu za mkononi inazidi kukua ndio maana tumeona umuhimu wa kuwa na kozi mbalimbali kwa ajili ya mafundi simu ili kuwe na watu wenye ujuzi katika sekta hii,” amesema Mdachi.

Hata hivyo kiongozi wa utafiti uliofanywa na DIT Dk. Petro Tesha nae alisema utafiti huo ulihusisha mafunzi kutoka mikoa ya Morogoro pamoja na Dar es salaam na ulikua na lengo la kubaini mapungufu na kutengeneza mtaala kwa ajili ya kuyaondoa matatizo hayo. ikiwa pamoja na kuangalia mazingira ya kazi ya mafundi hao, utaalamu pamoja na ujuzi wa sheria.

Akiwasilisha matokeo ya utafiti huo, Mkuu wa Chuo cha Veta Kipawa, Mhandisi Lutenganya Lucius, amesema wamebaini kuwa mafundi wengi hawakupata mafunzo rasmi ya taaluma ya utengenezaji simu wakati matokeo hayo yakionyesha asilimia 54 ya mafundi walipata mafunzo lakini asilimia 80 ya mafunzo hayo hayakuwa rasmi na asilimia 20 hawakupata kabisa mafunzo.

Mjumbe wa kikosi hicho, Dk. Paul Fahamuel kutoka DIT, amesema mtaala tayari umekamilika na kozi hiyo itatolewa kwa muda wa miezi mitatu na itanza kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa Video.

Chanzo : Mwananchi

9 comments
  1. Amosiignas
    Mimi jaman naitaji kusomea kuzi ya ufundi cm mana hii aidia ninayo hua natengeneza cm redio sasa naitaji kujiendeleza zaidi naomba mnisaidie hi kozi mwaka Hua ni Bei gani

  2. Naitwa Magembe frank toka Tanga mi Ninaaidia hiyo toka nasoma Darasa la 5 shule ya msingi Korogwe kwasemangube nikiwa na umri was miaka 15 hadi Leo hii natengeneza cm ila bado elimu ya ufundi cm sijaipa bado na ikiwa tayali nami ntaiji kujiunga na chuo hicho namba zangu ni 0715957125//0745283379

  3. Naitaji Kusoma Kozi Ya Ufundi Simu,Mimi ni Fundi Tiyari Na nina ofisi yangu.Ila Sijasomea na naitaji kusoma,Nawezaje Kupata iyo kozi?

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use