in

Hizi Ndio Simu Zitakazo Pata Toleo Jipya la Android 8.0 Oreo

Toleo jipya la Android limetoka na hizi ndizo simu zitakazo support

Ni siku chache zimepita toka toleo jipya la Android 8.0 Oreo kutoka rasmi, toleo hilo jipya linakuja na maboresho mengi sana na linategemewa kuwa moja kati ya toleo lenye ulinzi zaidi kuliko matoleo mengine ya mfumo wa Android.

Lakini kwa bahati mbaya sio kila simu itapata uwezo wa kuwa na toleo hilo jipya la Android Oreo au Android 8.0 na hii inatokana na uwezo wa simu kuweza kufanya kazi au ku-support mfumo huo.

Kwa mujibu wa Google ambao ndio watengenezaji wa mfumo huo hadi kufikia mwezi August mwaka huu ni simu chache karibia asilimia 12.3% ambazo zilikuwa zinatumia mfumo uliopita wa Android N au Android 7.0 ambao ndio mfumo unao tumika kwenye simu nyingi mpya za sasa.

Hata hivyo sababu ni asilimia chache sana ya simu ambazo zinatumia mfumo huo basi google imetangaza simu chache ambazo zitapata mfumo huo mpya wa Android 8.0 Oreo huku simu zingine zikiendelea kutumia mfumo wa zamani ili uweze kuzoeleka zaidi na watumiaji.

Jiandae na Samsung Galaxy S20 na Galaxy Fold 2 (February 11)

Zifuatazo ndio simu zitakazoweza kutumia mfumo huo mpya, simu zingine mpya zitakazokuwa zinatoka kuanzia mwezi ujao zitakuwa na mfumo huo wa Andorid 8.0 mpya moja kwa moja.

Simu za Google

Simu za Nokia Android

Simu za OnePlus

 • OnePlus 5
 • OnePlus 3
 • OnePlus 3T

Simu ya Essential Phone

Simu za HTC

Simu za Samsung

Simu za Sony (bado haujasibitishwa)

 • Xperia XZ Premium
 • Xperia Xzs
 • Xperia XZ
 • Xperia X Compact
 • Xperia X Performance
 • Xperia XA1
 • Xperia XA1 Ultra

Simu za LG

 • LG G6
 • LG Q6
 • LG G5
 • LG V20
 • LG V30

Hizo ndio simu ambazo mpaka sasa zinatarajiwa kuja na toleo jipya la Android 8.0, lakini kwa upande wa sony bado kampuni hiyo haijatoa taarifa kamili kuhusu kuja kwa toleo hilo kwenye vifaa vyake vya Android.

Kampuni ya Apple Yazindua Simu Mpya ya iPhone SE (2020)

Kwa sasa unaweza kudownload toleo la Android 8.0 kwa vifaa vya Google kupitia Link Maalum hapa. Maelezo kamili jinsi ya ku-install yana patika kwenye ukurasa huo.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa Video.

Chanzo : India Today

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.