Simu Mpya Zinazo Tarajiwa Kutoka Kuanzia Mwezi August 2017

Hizi ndio simu ambazo unatakiwa kuzingoja kuanzia mwezi huu.
SIMU ZINAZOKUJA SIMU ZINAZOKUJA

Baada ya kutoka simu mpya ya Samsung Galaxy Note 8, bado kuna simu kibao ambazo zina tegemewa kutoka kuanzia mwezi huu je ungependa kuzijua.? Basi kama ungependa kuzijua simu hizo basi uko mahali sahihi, twende moja kwa moja tukangalie simu hizo.

  • LG V30 – Tarehe 31 August

LG V30 imesha tangaza kuwa inategemea kutoa simu yake mpya tarehe 31 mwezi huu, simu hii inatarajiwa kuja na maboresho mazuri zaidi ikiwa pamoja na uwezo mkubwa wa kupiga picha.

  • Motorola Moto X4 – October (tarehe haijajulikana)

Kampuni ya Motorola kupitia watengenezaji wake wa simu Lenovo wamepanga kutoa toleo jipya la simu ya zamani ya Moto X simu hiyo inasemekana kuwa ni Moto X4 ambayo itakuja na sifa mbalimbali kama kioo cha inch 5.2 pamoja na processor ya Qualcomm Snapdragon 630, kumbuka pia motorola tayari walisha toa simu yao mpya ya Moto Z2 Force.

Advertisement

  • Sony Xperia XZ1 na XZ1 Compact – September (tarehe haijajulikana)

Kampuni ya Sony tayari imesha thibitisha kuja na simu zake mpya za Sony Xperia XZ1 pamoja na Sony XZ1 Compact, simu hizi ni matoleo mapya ya simu za Sony Xperia XZ. Kwa sasa bado hajajulikana simu hizi zitakuja na sifa gani tuendelee kusubiri kujua zaidi.

  • Huawai Mate 10 – Tarehe 16 October

Huawei tayari ilisha tangaza kwa umma kuwa inategemea kutoa simu mpya ya Huawei Mate 10 ambayo kwa mujibu wa tovuti ya bloomberg inasema simu hiyo itakuwa na nguvu kuliko simu zote ambazo zimewahi kutokea kwa kampuni hiyo ya Huawei. Na bado hakuna sifa kamili za simu hiyo zilizo julikana mpaka sasa bali kwa sasa kuna tetesi mbalimbali kuhusu simu hiyo.

  • HTC Ocean Life / HTC U11 Mini – Desember (tarehe haijajulikana)

HTC imesha tangaza kuja kwa toleo jipya la HTC 11 Ocen simu ambayo ilitoka mwanzoni mwaka huu, Hata hivyo HTC imepanga kutoa toleo hilo jipya la simu hiyo ambayo sasa itakuja na jina la HTC U11 Mini ikiwa na sifa kama processor ya Qualcomm Snapdragon 660 processor, kioo cha inch 5.2 chenye teknolojia ya Full HD display. Vilevile simu hii inatarajiwa kuja na kamera ya mbele na nyuma zote zikiwa na megapixel 16 pamoja na uwezo wa battery wa 2600mAh.

  • Apple iPhone 8 na iPhone 8 Plus – September 2017 (tarehe haijajulikana)

Tayari kumesha anza kutoka tetesi mbalimbali za simu mpya ya iPhone 8 ikiwa pamoja na video ya simu hiyo lakini bado hakuna sifa ambazo zime thibitishwa moja kwa moja lakini simu hiyo inategemewa kuja na maboresho makubwa sana ikiwa pamoja na uwezo wa kuchaji wireless pamoja na vitu vingine mbalimbali, ukichangia kuwa tayari toleo jipya la iOS 10.3.3 limesha toka.

  • Google Pixel 2 – October (tarehe haijajulikana)

Google inatarajia kuzindua toleo lake la pili la simu mpya ya Google Pixel, simu hii ya Google Pixel 2 ni moja kati ya simu ambazo zinazo subiriwa kwa hamu baada ya iphone 8 ukizingatia Android ni zao la kampuni ya Google tegemea mambo mengi sana kwa simu hii hasa kwa upande wa mzima wa mfumo wa uendeshaji.

  • Microsoft Surface Phone – Desember (tarehe haijajulikana)

Bado hakuna habari nyingi kuhusu simu hii mpya kutoka kampuni ya Microsoft, lakini tetesi mbalimbali zinasema huenda simu hiyo ikatoka kabla ya mwisho wa mwaka huu 2017 hivyo tuendelee kusubiria.

Na hizo ndio simu ambazo unaweza kuzipata kwa kipindi kiulicho baki cha kuanzia mwezi huu hadi kufikia mwisho wa mwaka, kumbuka simu hizi zinaweza kuwahi au kuchelewa kidogo kulinganisha na tarehe au mwezi ulio andikwa hapo juu.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa Video.

2 comments
  1. I am not sure where you are getting your information, but good topic.
    I needs to spend some time learning much more or understanding more.
    Thanks for great info I was looking for this information for my mission.wholesale mlb jerseys

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use