Kampuni ya simu na vifaa vya kieletroniki ya LG leo imetoa ripoti za ujio wa toleo jipya la simu yake ya LG V30, toleo hili ni toleo la juu ya toleo la LG V20 simu ambayo ilitoka hapo mwaka jana 2016.
Kupitia tovuti ya techradar LG imethibitisha kuwa simu hiyo itatoka rasmi tarehe 31 ya mwezi huu. Simu hiyo ambayo inatoka mwezi mmoja na Samsung Galaxy Note 8 inatarajiwa kuja na kamera kubwa yenye uwezo wa zaidi huku ikiwa na lensi mbili kubwa zenye uwezo wa kuchukua picha angavu sana.
Hata hivyo hayo yamethibitishwa na tovuti ya Techradar baada ya kupokea mualiko wa kudhuria uzinduzi huo ambao utafanyi hapo mwisho wa mwezi huu. Kwa mujibu wa tovuti ya phonearena LG V30 inatarajiwa kuja na sifa zifuatazo.
- Mfumo wa Uendeshaji Android 7.1.1 Nougat yenye LG UX 6.0
- Kioo Inch 6.0″ AMOLED 18:9 display 1440 x 2880 pixel Quad HD++ support for HDR content
- Ukubwa wa Simu Weight 151.4 x 75.2 x 7.4mm, Uzito bado haujajulikana
- Kamera za Nyuma 13MP + 13MP (super wide-angle), Kamera ya mbele haija julikana.
- Ukubwa wa Ndani 64GB + microSD
- Uwezo wa Battery 3,000 mAh with USB-C
Tetesi pia zinasema simu hiyo itakuja bila pini ya headphone maarufu kama headphone jack, badala yake itakuwa inatumia headphone zenye kutumia USB type c, lakini itabidi tusubiri tarehe 31 ili tuweze kujua na kudhibitisha kuhusu hili.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.
Chanzo : Techradar