Hivi karibuni umesikia sana jina la Essential Phone, hii ni kwa sababu hii ndio aina mpya ya simu kwa sasa na ni gumzo sana mtandaoni na pengine ndio sababu ya kukuletea sifa za Essential Phone hii ambayo imeingia sokoni rasmi hapo jana.
Kwa ufupi kabisa ni vyema kujua historia fupi ya simu hii kwani ili kuipenda na kujua ubora wake kwa undani ni vyema ujue simu hii ilipotoka. Kwa kuanza basi ni vyema ujue kuwa Essential Phone ni moja ya simu ambazo zimebuniwa na muanzilishi na mbunifu wa mfumo wa uendeshaji wa Android Andy Rubin.
Kwa mujibu wa tovuti ya Wikipedia, Andy pamoja na wenzake watatu ndio waliokuwa wanzilishi wa kampuni ya Android Inc, ambayo ilikua ikitengeneza mfumo wa uendeshaji wa Android, lakini mfumo huo ulinunuliwa na Google mwaka 2005 kitendo kilichomfanya Andy kuendelea kuwa kiongozi wa makampuni mengine mbalimbali.
Hadi kufikia mwaka 2017 Andy alikua kiongozi wa makampuni mbalimbali ikiwa pamoja na kampuni ya Essential Products Inc, kampuni mpya ya mwaka huu 2017 ambayo ndio iliyotoa simu hii mpya ya Essential Phone ambayo ndio tunangalia sifa zake siku ya leo.
Baada ya kusema hayo basi moja kwa moja twende tuka angalie sifa za Essential Phone simu hii mpya kutoka kwa muanzilishi wa Android. Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali huwenda simu hii ikawa ndio mshindani mkubwa wa simu mpya ya Samsung Galaxy S8.
HIZI HAPA NDIO SIFA ZA ESSENTIAL PHONE
- Mfumo wa Uendeshaji Android 7.1.1
- Kioo 5.7-inch LCD, 2560×1312 (505 ppi)Corning Gorilla Glass 5
- Uwezo wa Processor Qualcomm Snapdragon 835 2.45GHz octa-core Kryo 280 CPU Adreno 540 GPU
- RAM 4GB
- Ukubwa wa Ndani 128GB (UFS 2.1) Non-expandable
- Kamera ya Nyuma Dual 13MP camera (color + monochrome) f/1.85 lens, phase-detect + laser auto focus 4K video at 30fps, 1080p at 60fps or 720p at 120fps
- Kamera ya Mbele 8MP with f/2.2 lens 4K video at 30fps, 1080p at 60fps or 720p at 120fps
- Battery 3040mAh Non-removable
- Sehemu ya Kuchaji Charging USB-C fast charging
- Water resistance No
- Muunganisho 802.11ac Wi-Fi with MIMO, Bluetooth 5.0 LE
- NFC, GPS and GLONASS
- Vifaa vya Ziada power pins with 6 Gbps wireless data transfer
- Finger Printi Security One-touch rear fingerprint sensor
- Sehemu ya Chaji USB-C to 3.5 mm headphone adapter included
- Rangi Colors Black Moon, Pure White, Stellar Grey, Ocean Depths
Na hizo ndio sifa za simu mpya ya Essential Phone iliyotoka hivi karibuni, simu hii kwa sasa inauzwa dollar za marekani $699 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 1,565,340.60 kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya leo, simu hii inakuja na vitu vya pembeni kibao natumaini umesha angalia video hapo juu hivyo utakua unalijua hilo…
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.